Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wakazi Kijiji cha Kimondolosi Kata Olasiti
Wilaya ya Arusha mjini.
Mkuu wa Mkoa Arusha,
Mrisho Gambo (kushoto) akizungumza na wakazi wa Kimondolosi, wilaya ya Arusha
mjini, wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (katikati) ya
kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini (REAIII) wilayani
humo.
Wakazi wa Kata ya
Olasiti, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani aliyekuwa
akizungumza kuhusu kuwapatia huduma ya umeme.
Waziri wa Nishati,
Dkt.Medard Kalemani (wa Tatu kushoto) akikagua nguzo za umeme katika Kata
ya Terati, zitakazotumika kuwapatia Umeme wananchi wa eneo hilo mkoani
Arusha. Wa Pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Na Zuena Msuya,
Arusha
Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi mmoja kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
kuhakikisha kuwa vijiji vyote vilivyopo katika Jiji la wa Arusha vinaunganishwa
na huduma ya umeme.
Dkt. Kalemani alitoa
agizo hilo jijini Arusha baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa
kusambaza umeme vijijini (REA III) katika Vijiji vilivyopo jijini humo na
kujionea hali ya ukosefu wa nishati ya umeme.
Dkt. Kalemani alisema
kuwa, Wananchi hawafurahii kucheleweshewa kupata huduma ya umeme hali ya
kuwa wengine walikwishalipia huduma hiyo.
" Haipendezi na
haifurahishi machoni mtu kajitahidi kujibana na kujenga nyumba yake nzuri na ya
kisasa, lakini anakosa umeme wakati uwezo wa kumuunganishia upon a vifaa vipo,
sasa kwa nini asiunganishwe.?," alihoji Dkt. Kalemani.
Kutokana na hali hiyo,
aliwataka TANESCO kuunda vikosi kazi mbalimbali vitakavyosaidia kazi ya
kusambaza umeme kwa wananchi kwa haraka.
Aidha, alimwagiza
mkandarasi anayesambaza umeme jijini humo, kampuni ya Nipo Group, kuhakikisha
kuwa anawafungia umeme wananchi wa Kimondorosi katika Kata ya Olasiti
mkoani Arusha na kuhakikisha kuwa kila siku anatoa ripoti ya
utekelezaji wa mradi kwa mtendaji wa mtaa huo hadi atakapomaliza kuweka
umeme kwa wananchi.
Alisema kuwa,
mkandarasi huyo anapaswa kufanya kazi hiyo ili kuwaondolea kero ya ukosefu wa
umeme wananchi hao ambao wamekaa kwa muda mrefu bila kupata huduma hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo alimshukuru Waziri wa Nishati kwa kutoa agizo hilo
litakalopelekea wananchi hao kupata umeme kwani wananchi hao walishamlalamikia
kuhusu kukosa huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment