Wananchi wamehamasishwa kuimarisha ulinzi ili kujilinda wao wenyewe na mali zao
dhidi ya watu wenye nia ovu
Hayo yamesemwa na
mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati wa muendelezo wa
ziara yake katika kata za Kahama na Shibula juu ya kukagua miradi
inayotekelezwa ndani ya jimbo hilo, kusikiliza kero na changamoto, kuhamasisha
utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kuzungumza na watumishi wa umma,
wastaafu, viongozi wa dini, viongozi wa mitaa na wazee maarufu ambapo
amewahamasisha wananchi wa kata hizo kuhakikisha wanashiriki katika kutekeleza
wajibu wao wa kujilinda na kulinda mali zao dhidi ya watu wenye nia ovu badala
ya kuachia jeshi la polisi peke yake kitendo ambacho kinachangia kutokea kwa
matukio ya kihalifu maeneo tofauti tofauti ya jimbo hilo
‘… Kulikuwa na
utaratibu wa kujilinda kupitia mitaa yetu suala hili limeishia wapi?, Kwasababu
wewe ukilala ndani unastarehe ukafikiri askari nane watalinda watu laki mbili
ni ngumu …’ Alisema
Aidha Dkt Mabula
amewaasa wananchi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa
kutoa taarifa sahihi za vitendo vya kihalifu vinavyofanyika ndani ya maeneo yao
na kuwafichua watu wote wanaoonekana kuwa na nia ovu ya kutekeleza matukio hayo
kwani jukumu la kulinda usalama wa raia na nchi kwa ujumla ni jukumu la kila
mtu na si serikali peke yake kama inavyoelekeza katiba ya nchi ya Tanzania.
Mhe Mabula pia
amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo ndani ya jimbo lake
kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati huku akisisitiza kuwa
hatavumilia uzembe wowote utakaosababisha kukwama kwa miradi hiyo sambamba na
kuwaomba wananchi wa kata ya Kahama kuhakikisha wanatumia nafasi za ajira
zinazojitokeza kupitia utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo.
Kwa upande wake
afisa mipango miji wa manispaa ya Ilemela ndugu Kennedy Chigulu akijibu hoja
zilizojitokeza kutoka kwa wananchi kupitia ziara hiyo amewataka wananchi
kuhakikisha hawajengi kiholela kwa kufuata sheria na taratibu za mipango miji
ikiwa ni pamoja na kutovamia maeneo ya jeshi kutokana na sababu za usalama wa
nchi huku akiwahakikishia kuwa manispaa ya Ilemela kupitia wizara ya ardhi
imeendelea kutatua kero za ardhi wakati wizara ya ulinzi ikijipanga kulipa
fidia kwa maeneo yote stahiki iliyoyatwaa na hivyo kuwa wavumilivu wakati madai
yao yakifanyiwa kazi.
Ziara hiyo
iliongozwa na mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ambae pia ni Kaimu mkuu
wa wilaya ya Ilemela Mwl. Khadija Nyembo na kuhudhuriwa na watalaamu wote wa
manispaa ya Ilemela wakiongozwa na Mstahiki Meya wa manispaa Ilemela Mhe
Renatus Mulunga, Kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo ndugu Daniel Batare, Katibu
siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Ilemela na diwani wa kata ya Kahama.
' Ilemela ni yetu,
tushirikiane kuijenga'
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
10.07.2018
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
10.07.2018
0 comments:
Post a Comment