Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania iliyofanyika TARI-SERIAN Jijini Arusha leo tarehe 21 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya watafiti kutoka vituo mbalimbali vya utafiti Tanzania-TARI wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania iliyofanyika TARI-SERIAN Jijini Arusha leo tarehe 21 Julai 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikata utepe kuzindua Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania iliyofanyika TARI-SERIAN Jijini Arusha leo tarehe 21 Julai 2018. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi TARI Dky Yohana Budeba (Katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza na watafiti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania iliyofanyika TARI-SERIAN Jijini Arusha leo tarehe 21 Julai 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi TARI Dkt Yohana Budeba vitabu vya sheria ya kuanzisha TARI wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania iliyofanyika TARI-SERIAN Jijini Arusha leo tarehe 21 Julai 2018.
Na Mathias Canal-WK, Arusha
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amewapongeza watafiti wa
kilimo kote nchini na kuwataka kutoa matokeo ya tafiti wanazozifanya kwa
muktadha wa kujibu mahitaji ya wakulima, wafanyabiashara na jamii kwa ujumla.
Alisisitiza kuwa utafiti ni suala la msingi katika maendeleo ya Taifa
kwa kuwezesha uimarishaji wa mnyororo wa thamani kwani utafiti ukijibu hoja za
wakulima sekta hiyo itaimarika zaidi na hivyo kuongeza tija katika uzalishaji
wa mazao mbalimbali nchini.
Dkt Tizeba ameyasema hayo leo tarehe 21 Julai 2018 wakati wa hafla
ya uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania iliyofanyika
TARI-SERIAN Jijini Arusha.
Alisema kuwa nchini Tanzania sekta ya kilimo inachangia asilimia 30%
ya pato la Taifa na kutoa ajira kwa zaidi ya asilimia 65% mpaka asilimia 70% hivyo
watafiti hao wanapaswa kuongeza tija katika ufanisi wa utafiti wao ili
kuwanufaisha wakulima.
Halikadhalika ameeleza kuridhishwa kwake na kazi zinazofanywa na watafiti
nchini na kutumia fursa hiyo kuwapongeza kwa kazi nzuri waifanyayo ambayo
imechangia kuongeza tija katika kilimo,“Pamoja na kuwapongeza lakini mnapaswa
kutambua kuwa Wizara ya kilimo ndiyo inaongoza kwa kuwa na wasomi wengi lakini
bado changamoto ya kubadili mtazamo kwa wakulima ili kuzalisha mazao yao kupitia
mbinu bora za kilimo cha kisasa” Alisema
Alisema kuwa lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ni kuona wakulima wanaishi maisha bora na wanachangia katika suala zima la kuwa
na maisha bora hivyo endapo kama watafiti watawajibika ipasavyo sekta ya kilimo
itakuwa zaidi na kabla ya mwaka 2025 Tanzania itafikia uchumi wa kati.
Wakati huo huo waziri huyo wa kilimo, ameagiza idara ya
uhawilishaji wa teknolojia na mahusiano katika Taasisi
ya Utafiti wa kilimo
Tanzania (TARI) kuongeza tija
katika kuzitangaza mbegu mbalimbali zinazozalishwa na TARI ikiwemo mbegu ya
Mahindi Lishe aina ya HK1 ambayo ina mwaka wa tisa mpaka sasa tangu izalishwe
ilihali wananchi hawaifahamu.
Aidha, amewasihi watafiti hao kutokuwa watafiti
wa maandishi badala yake kuwa watafiti wa kuwanufaisha wananchi huku akiongeza
kuwa taasisi za utafiti zinapaswa kufanya biashara ili ziweze kujiendesha na
kupunguza mzigo wa tegemezi kwa serikali.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment