METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, June 5, 2018

WATEMI WA KISUKUMA WAOMBA KUREJESHWA KWA FUVU LA MTEMI WA BUJASHI

Watemi wa kisukuma wameomba kurejeshwa nchini kwa fuvu la mtemi wa Bujashi lililopo nchini Ujerumani.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa watemi wa Kisukuma Chifu Charles Hale wakati wa ufunguzi wa tamasha la jadi, mila, na desturi za kabila la Kisukuma Bulabo ambalo hufanyika kila mwaka kusheherekea sikukuu ya mavuno linaloenda sambamba na ibada ya Karista takatifu ya kanisa Katoriki iliyofanyika katika kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma BUJORA kilichopo Kisesa wilayani Magu mkoa wa Kwanza.

'... Tunaipongeza Serikali kwa kufanikisha kurejeshwa nchini kwa fuvu la mtemi Mkwawa, Tunaomba na fuvu la mtemi wa Bujashi lililopo nchini Ujerumani nalo liweze kurejeshwa ...' Alisema

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe Dkt Harrison Mwakyembe mbali na kupokea ombi hilo ameahidi kukifanyia maboresho kituo hicho cha utamaduni na kuongeza kuwa wizara yake itaendelea kushiriki sherehe hizo za kila mwaka kama ishara ya kuunga mkono jitihada za kulinda na kudumisha mila na utamaduni nchini.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufika kilele siku ya Jumapili June 10, 2018 katika viwanja vya Michezo Kisesa wilaya ya Magu lilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula, Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe Kiswaga, Mkuu wa mkoa Mwanza Mhe John Mongela na viongozi wengine mbalimbali.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com