Meneja
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akionesha kadi ya uanachama wa mfuko huo alipokuwa akizungumza na
wajasirimali kwenye kongamano lililofanyika ukumbi wa
vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma
Meneja
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akizungumza na
wajasiriamali katika kongamano lililofanyika ukumbi wa
vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma
Wajasiriamali wakiwa
kwenye kongamano uliofanyika jana Jijini Dodoma ambalo liliandaliwa na Mfuko wa NSSF.
..............................................................
MFUKO wa Hifadhi ya
Jamii(NSSF) umewashauri wajasiriamali nchini kujiunga kwenye vikundi ili
kuweza kutambuliwa na kupata mikopo.
Ushauri huo umetolewa
na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma wakati alipokuwa akitoa mada yake
kwenye Kongamano la Wajasiriamali lilifanyika jijini Dodoma.
Chuma amesema
wajasiriamali hao wakiunda na kuvisajili vikundi vyao watapata mikopo kutoka
NSSF ili kukuza biashara zao.
Amesema mfuko huo
hautaweza kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kwani masharti ya mikopo itatolewa
kupitia vikundi au Saccos mbalimbali zilizosajiliwa.
“Lengo la mikopo hii
ni kuunga jitihada za serikali katika kuwainua wananchi wa kipato cha chini
kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025,”amesema.
Pamoja na kupata
mikopo wajasiriamali hao, watapata fursa ya kujiunga na pia na kuchangia
michango katika mfuko huo jambo ambalo litawawezesha wanachama kunufaika na
mafao yanayotolewa na NSSF.
Alitaja baadhi ya
mafao hayo kuwa ni fao la Afya linalomwezesha mwanachama aliyejiunga kupata
huduma za afya na mafao mengine kusaidiwa wakati wa majanga ya ajali au msiba.
Kwa upande wake mgeni
rasmi katika kongamano hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na
Vijana Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali hao kuwa waaminifu katika
kuchukua na kurejesha mikopo hiyo ili na waweze kukopeshwa.
0 comments:
Post a Comment