Na
Munir Shemweta, Nachingwea
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ameziataka
Halmashauri nchini kutenga maeneo ya ujenzi wa nyumba za watumishi yenye miundombinu
ili shirika la nyumba la taifa (NHC) liweze kujenga nyumba za gharama nafuu.
Mhe
Mabula amesema hayo jana wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake
mkoani Lindi kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na kuhamasisha
ulipaji kodi za ardhi kwa wananchi wa mikoa ya lindi na Ruvuma.
Alisema,
Shirika la Nyumba la Taifa halitakiwi kuingia gharama ya kutafuta maeneo pamoja
na kuweka miundombinu kwani kwa kufanya hivyo kutalilazimu shirika kujenga
nyumba na kuziuza kwa gharama kubwa jambo litakalowafanya watumishi na watu
wengine wanaozihitaji kushindwa kuzinunua au kupanga.
‘’NHC
haitakiwi kuingia ghrama zozote, halmashauri ndiyo inapaswa kutenga maeneo na
kuhakikisha huduma zote muhimu kama maji, barabara, umeme vinakuwepo na Shirika
kazi yake iwe kujenga nyumba tu’’ alisema Mabula
Alibainisha
kuwa, iwapo halmashauri zitatenga maeneo na kupeleka huduma zote muhimu basi
shirika la nyumba litaweza kujenga nyumba kwa gharama ndogo na kuziwezesha halmahauri
kuwa na nyumba zake ambazo zinaweza kuuzwa au kuwapangishwa na kubaki kama
rasilimali ya Halmashauri.
Amelitaka
shirika la nyumba la Taifa kuhakikisha linaingia makubaliano ya ujenzi wa
nyumba na halmashauri kwanza kabla ya kuanza ujenzi ili kuepuka kujenga nyumba zitakazokosa
mnunuzi kama ilivyojitokeza kwa baadhi ya maeneo jambo linalolipa hasara
shirika la nyumba.
‘’kuna
maeneo halmashauri zimejengewa nyumba na shirika lakini hazijauzwa sasa
utawezaje kujenga nyingine wakati ulizojenga awali hazijauzwa? ‘’ alihoji Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mabula
ameisifu halmashauri ya Uyui kwa kujengewa nyumba na Shirika la Nyumba la Taifa
na kuzinunua zote 32 ilizojengewa jambo alilolielezea kuwa ni mfano wa kuigwa
na halmashauri nyingine.
Kwa
mujibu wa Mabula, malengo ya shirika katika ujenzi wa nyumba ni kuuza, kupangisha
na kuwa na mpangaji mnunuzi jambo alilolieleza kuwa linalisaidia shirika kupata
fedha za kujiendesha na wakati huo kuwezesha wananchi kuwa na makazi bora.
Kwa
upande wake, meneja wa shirika la nyumba la taifa mkoa wa Lindi Gibson
Mwaigomole amesema shirika lake limekuwa likizungumza na halmshauri za mkoa huo
lengo likiwa kuhakikisha wanajenga nyumba kwa ajili ya kuziuza kwa halmashauri.
Hata
hivyo, Alisema baadhi ya halmashauri zimekuwa na uhitaji wa nyumba na na tayari
wamezungumza nazo na kutolea mfano wa Halmashauri ya manispaa ya Lindi kuwa ni
moja ya halmashauri za mkoa wa Lindi iliyoomba kujengewa 54.
0 comments:
Post a Comment