METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 29, 2018

ILEMELA KUNUFAIKA NA PESA ZA UJENZI WA HOSPITALI ZA WILAYA

Wilaya ya Ilemela imekuwa miongoni mwa wilaya 67 nchini zitakazonufaika na mgawo wa fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya nchini baada ya kukosekana kwa huduma hiyo tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo

Mafanikio hayo yamekuja kufuatia juhudi kubwa na ushirikiano kati ya wananchi, watumishi na viongozi wa wilaya hiyo chini ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula mapema mwaka huu alipoomba kusaidiwa kukamilishwa kwa hospitali hiyo, kusaidia upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu alipofanya ziara ya kukagua kituo cha afya cha Karume kilichojengwa ndani ya wilaya hiyo

Mara baada ya ombi hilo kutoka kwa mbunge wa Jimbo la  Ilemela, Waziri huyo wa Afya aliahidi kusaidia kukamilika kwa hospitali hiyo ya wilaya ikiwa ni pamoja na kutoa fedha nyengine kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Buzuruga ili kukifanya kuwa cha kisasa zaidi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi ahadi ambayo imekwisha tekelezwa ikiwa zaidi ya milioni mia nne zimekwisha tolewa na kupokelewa kwaajili ya kuanza ujenzi huo

Kwa upande wake Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli kupitia kwa Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Suleiman Jafo kwa kusaidia kumaliza kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wananchi wake, Pia amewaomba wananchi wa jimbo hilo na viongozi wengine kuendelea kushirikiana na kuunga mkono jitihada zote zinazochukuliwa katika kuhakikisha wanapata maendeleo ya haraka huku akiwaahidi kuendelea kuwatumikia kwa nguvu zake zote na muda wote kuhakikisha wanafikia malengo.

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’ 

Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
29.06.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com