METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, April 12, 2018

MD KAYOMBO AREJESHA UMILIKI WA VIBANDA 297 NA VIZIMBA VYA MANISPAA YA UBUNGO

Hayo yamejiri leo tarehe 12/04/2018 ambapo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ndg.John L.Kayombo alipofanya ziara katika soko la Shekilango kwa nia ya kusikiliza kero za wafanyabiashara, wamiliki na wapangaji wa vibanda na kuzungumza nao masuala ya kibiashara.

Mkurugenzi aliambatana na wataalam kutoka Manispaa akiwemo Mhandisi, Afisa Ardhi, afisa mipango miji na Mwanasheria ambapo kila mmoja kwa eneo lake walipata fursa ya kutoa ufafanuzi katika masuala mbalimbali ambayo wafanyabiashara walitaka kufafanuliwa.

Akiongea  Mkurugenzi kuhusu mipango mbalimbali iliyopo juu ya soko hilo alisema "Manispaa kwa fedha zake za ndani ina mpango wa kujenga soko la kisasa katika eneo hilo ambalo litakuwa la mfano na tayari utambuzi wa mipaka umeshaanza kufanyika kwa ajili ya utekelezaji.

Kuhusu uboreshwaji wa choo amemuagiza injinia wa manispaa na timu yake kufika na kuangaliakids namna ya kuboresha choo hicho na kufanyia ukarabati kazi hiyo itaanza mara moja na itaenda sambamba na kushughulikia kero walizowasilisha ikiwemo na mfumo wa maji taka yanayotokana na machinjio ya kuku na uboreshaji wa soko kwa jumla.

Alisema kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja, miezi minne na siku 12 ambazo yeye ameitumikia Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,kwa upande wa masoko ameweza kujenga masoko manne ya mboga mboga kwa makusanyo ya ndani.

Aliongeza kwamba nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili iweze kukusanya kodi na hatimaye kupata mapato

Aidha katika hatua nyingine ndg. Kayombo alisema kwamba kwa muda mrefu Manispaa imepoteza mapato yake kupitia kodi za vibanda. Alisema tayari anazo taarifa kuwa kuna watu walijimilikisha vibanda hivyo miaka ya nyuma kinyume cha sheria ambapo wamekuwa wakiilipa halmashauri kodi ya Tshs.15000 kwa mwezi sawa na Tshs.180000 kwa mwaka  ambapo wao huwapangisha wafanyabiashara wengine  kwa kodi ya Tshs.*200000* hadi *300000* kwa mwezi sawa na Tshs *2400000* hadi *3600000* kwa mwaka hivyo hupelekea Halmashauri kupata fedha kidogo wakati wao hupangisha kwa kiasi kikubwa cha fedha.kutokana na hilo
'Kuanzia leo tarehe 12 mwezi wa 4 siku ya Alhamisi vibanda na vizimba vyote ni mali ya Manispaa na vitakuwa chini ya Mkurugenzi" Alisisitiza Kayombo.

Aliagiza wapangaji wote waliokuwa wakilipa kodi ya vibanda halmashauri v  na wapangaji waliowapangisha wao kufika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliyopo Kibamba siku ya Alhamisi tarehe 19/4/2018 saa 2 kamili asubuhi  wakiwa na mikataba ili kupewa utaratibu.

Aidha aliwatoa hofu wapangaji wote na kumwambia kuwa biashara zao ziko salama na wataendelea kutumia vibanda vya Halmashauri baada ya kupewa utaratibu na maelekezo.

Pia Mkurugenzi aliwataka wafanyabiashara wote kufanya biashara kwa amani ili kujipatia kipato na yeye kama kiongozi wao yupo nyuma yao.Pia alisisitiza kutoleta mambo ya siasa mahali pa Biashara.

Huu ni muendelezo wa ziara za Mkurugenzi Kayombo ambapo kesho 13/4/2018 atakuwa katika soko la Sinza Makaburini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com