Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi.
Mkoa wa
Geita unatarajia kunufaika na mradi kabambe wa usambazaji umeme vijijini REA
awamu ya Tatu kwa kuongeza shughuli za kiuchumi kwa wananchi kutokana na
vitongoji 220, vijiji 372 na Kata 499
ambazo zinatarajia kunuifaika na Nishati ya Umeme.
Akizungumza
mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim
Ruweta amesema Mradi huo kwa mzunguko wa
kwanza utaunganisha wateja wapatao 12,944 na hivyo kukamilika kwa Mradi huo utafanya
umeme kuongezeka kwa Asilimia 51 kwa wateja waliopo sasa.
“Mategemeo
yetu ni kwamba mzunguko wa pili ambao unatarajia kuanza mwaka 2019 na
kumalizika mwaka 2020 na 2021 utafanya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita kupata
umeme kwa asilimia mia moja” Alisema Ruweta.
Kwa upande
wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wananchi kutoa
ushirikiano na kujua kuwa hakuna fidia ambazo watalipwa kutokana na mradi huo.
“Wito kwa
wananchi wa Mkoa wetu wa Geita watoe ushirikiano Katika vijiji vyote ambako
wataalamu wetu watapitia wajue kuwa hakuna fidia kwasababu mradi huu utakuja
kwaajili ya kutupatia maendeleo na unapowasha umeme itasaidia kukua kwa uchumi
wa eneo husika na Mkoa wetu” Alisema Luhumbi.
Aidha kwa
upande wake Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda alisema hadi sasa hivi bado hawajaona
tatizo lolote ambalo lipo kwenye mradi huo na kwamba wanaamini watafanikisha
kwenye maeneo yote ambayo mradio huo umepangwa kufanyika.
Mradi wa REA
awamu ya tatu mzunguko wa kwanza Mkoani Geita unatekelezwa na mkandarasi aitwaye
White city Guangdong JV ambaye ni ubia wa Kampuni ya Kitanzania na Kampuni ya nje
na unatarajia kugharimu zaidi ya Shilingi za kitanzania Bilioni 61 na fedha za
Kimarekani Dola milioni 7.8.
|
0 comments:
Post a Comment