Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)
Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiongea na wanawake waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza kwenye ziara ya UWT taifa mkoani Iringa katika Kata ya Mkwawa
Baadhi ya wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT katika kata ya Mkwawa wakatika wa ziara ya viongozi wa kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT katika kata ya Mkwawa wakatika wa ziara ya viongozi wa kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wakiwa katika kitendo cha kula kiapo pamoja na wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT kata ya Mkwawa
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)
Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo Pamoja katibu wa UWT manispaa ya Iringa
Na Fredy Mgunda, Iringa
MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)
Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan amevuna
wanachama wapya zaidi ya themanini (80) katika kata ya Mkwawa Manispaa ya
Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.
Wanachama hao
wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani
Iringa, ambapo MNEC Ramadhan
alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa kata ya Mkwawa ndipo waliposhawishika
kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa MNEC huyo.
Ramadhan alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama
ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia
mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu
katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.
“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi
Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake
kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana
ya kuongoza nchi hii” alisema Ramadhan
Aidha Ramadhan aliwataka wanawake kujifunza
kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio
wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.
“Wanawake wenzangu sasa
imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama
sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana
tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisema Ramadhan
Ramadhan alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya
biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya
bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa
maendeleo yako.
“Siku hizi kuna mabenk
mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha
hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia
kuinua maisha ya mtanzania” alisema Ramadhan
Ramadhan alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya
Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze
kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.
“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona
faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa
umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Ramadhan
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa atawapatia elimu ya
ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya
maendeleo.
“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali
mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida
na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu
mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Kabati
0 comments:
Post a Comment