Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde amewataka waajiri kuhakikisha wafanyakazi wao wanasajiliwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kama Sheria inavyoelekeza na kuwapa siku kumi na nne (14)kuwapa Wafanyakazi wote mikataba kwa mujibu wa *Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini Na.6/2004*
Mavunde ameyasema hayo leo huko Wilaya ya Mkuranga,Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sheria za Kazi,Sheria ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Aidha Mavunde amevitoza Faini Viwanda vya *TIAN TAN GROUP LTD-Tsh11,400,000,DILLION CO. LTD- Tsh14,000,000 na LN FUTURE BUILDING-Tsh7,000,000* kwa kukiuka *Sheria ya AFYA na USALAMA mahala pa kazi No.5 ya 2003.*
Wakati huo huo Mavunde pia ameuagiza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kuvifikisha Mahakamani Viwanda vya *T-SINO LTD,LN FUTURE BUILDING* na *TIAN TAN GROUP* kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh Alberto Sanga ameahidi kusimamia utekelezaji wa maaigizo ya Naibu Waziri Mavunde ili kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya kufanua kazi.
0 comments:
Post a Comment