Naibu Waziri madini Dotto Biteko(katikati mwenye kizibao
chekundu) akikagua bidhaa zinazozalishwa na mgodi wa mawe wa Udbhav
international Ltd uliopo kijiji cha Ntyuka manispaa ya Dodoma
alipotembelea jana katika ziara yake ya kawaida ya kikazi.
Mmiliki
wa mgodi wa mawe wa China Dragon Internation .co.Ltd Sist Mganga (wa kwanza kushoto)
akimpa maelezo naibu waziri wa madini Dotto Biteko (wa pili toka kushoto)
alipotembelea juzi mgodi huo uliopo Kijiji cha Itiso Wilaya ya Chamwino Mkaoni
Dodoma

Naibu Waziri Madini Dotto Biteko(katikati mwenye kizibao
chekundu) akikagua mashimo ya mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika
kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana kwenye ziara
yake ya kawaida ya kikazi.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wachimbaji wa mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana.
Naibu Waziri Madini Dotto Biteko(katikati mwenye kizibao
chekundu) akikagua mashimo ya mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika
kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana kwenye ziara
yake ya kawaida ya kikazi.
Naibu Waziri Madini Dotto Biteko(katikati mwenye kizibao
chekundu) akikagua mashimo ya mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika
kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana kwenye ziara
yake ya kawaida ya kikazi.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko akikagua machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha
Nholi Wilaya ya Bahi.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na
wachimbaji wa mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha
Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana.
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko ameagiza
kukamatwa kwa magari na vitendea kazi kwa kampuni za ujenzi wa barabara
zinazodaiwa fedha za mirabaha kwa kuwa zinatakiwa kulipa kwa mujibu wa sheria.
Biteko ametoa agizo hilo baada ya
kupewa taarifa na Afisa madini mkazi wa Dodoma Silimu
Mtigile kuhusu madai ya makampuni hayo wakati wa ziara ya siku ya moja
kutembelea migodi ya uchimbaji madini katika mkoa wa huo.
Amesema kampuni yeyote ya ujenzi wa
barabara inayodaiwa fedha za mirabaha na serikali haitaruhusiwa kuondoa mitambo
yake kwenye eneo kazi hadi itakapolipa.
Ameeleza kuwa kampuni hizo zinapaswa
kulipa madeni ya tozo mbalimbali wanazodaiwa na Serikali.
Hata hivyo Biteko amewataka wasimamizi
wa serikali katika kukusanya kodi hizo kuwa waaminifu na wasiisababishie
serikali hasara kwa kurubuniwa na wadaiwa.
Ameagiza Ofisi ya madini ikutane na wahusika
wa madeni hayo ya kodi ya madini katika maeneo yao ya kazi ili kutoa elimu
jinsi ya kulipa kodi hizo zinazostahili.
Awali katika taarifa aliyoitoa kwa
Naibu Waziri huyo, Afisa madini huyo amesema kuna baadhi ya wakandarasi wa
ujenzi wa barabara wanadaiwa deni la mirabaha ya ujenzi zaidi ya sh.
bilioni 1.9 na wameshalipa Sh.milioni 642.5.
Ametaja wakandarasi hao kuwa ni kampuni
ya Chico ilikuwa inajenga barabara ya Mayamaya hadi Mela , CRSG ambayo ilijenga
barabara ya Mela hadi Bonga, Sinohydro Company ambayo imejenga barabara ya
Dodoma mjini hadi Mayamaya na CCCC iliyojenga barabara ya Dodoma hadi Fufu.
Aidha amesema katika mwaka wa fedha wa
mwaka 2016/17 madini waliweka malengo ya kukusanya maduhuli ya serikali kiasi
cha sh.Bilioni 1.2 ambapo walivuka malengo kwa asilimia 120.34 kwa kukusanya
zaidi ya Sh.bilioni 1.4.
0 comments:
Post a Comment