Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda
akifunga Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK)
kwa wawezeshaji watakaowafundisha walimu wanaofundisha madarasa ya MEMKWA mjini
Morogoro leo, Kulia kwake ni Odilia
Mushi Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu (Elimu ya Watu Wazima) Ofisi ya
Rais TAMISEMI na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya
Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Syston Masanja amesema Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia iliwakabidhi Taasisi yao (ADEM).
Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda akiwa
katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma,
Kuandika, na Kuhesabu (KKK) kwa wawezeshaji watakaowafundisha walimu
wanaofundisha madarasa ya MEMKWA mjini Morogoro leo
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma,
Kuandika, na Kuhesabu (KKK) kwa wawezeshaji watakaowafundisha walimu
wanaofundisha madarasa ya MEMKWA wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa
ufunguzi wa mafunzo hayo mjini Morogoro
Na Fred J. Kibano
Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda
amefungua leo
Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu
(KKK) kwa
wawezeshaji watakaowafundisha walimu wanaofundisha madarasa ya
MEMKWA mjini
Morogoro.
Akifungua mafunzo hayo mjini Morogoro, Nzunda amewataka
washiriki hao kufanya
weledi, uadilifu, na uwajibikaji lakini pia kufanya tafiti
zitakazosaidia kuboreshwa kwa
Sekta ya Elimu nchini pamoja na kubadili fikra zao ili kuleta
matokeo makubwa.
“Fanyeni weledi, uadilifu, na uwajibikaji, kusimamia na kufanya
tafiti, lakini pia
tunategemea mafunzo haya yawabadilishe mwenendo, tabia, kifikra
na kimtizamo ili
muweze kwenda kuhamisha maharifa hayo kwa wengine na baadaye
muweze kuleta
mabadiliko makubwa ndani ya sekta ya elimu,”amesema.
Nzunda amewataka washiriki hao kuwa makini na wadadisi wakati
wote wa mafunzo ili
walimu watakaopatiwa mafunzo ya madarasa ya Mpango wa Elimu ya
Msingi Kwa
Wasiobahatika (MEMKWA).
“Nitoe wito kwenu washiriki wa mafunzo haya, kuwa makini na
wadadisi kwa madazote
zitakazowezeshwa ili nanyi mfikishe maudhui hay ohayo kikamilifu
kwa walimu
wanaofundisha madarasa ya MEMKWA,”amesema.
Nzunda ameyataja moja ya mafanikio ya MEMKWA ni pamoja na mwaka
2012 ilitoa wanafunzi 4170 waliochaguliwa kujiunga na darasa la tano na wengine
1576waliweza kujiunga na masomo ya sekondari.
Aidha, amesema licha ya ongezeko kubwa la watoto wanaoandikishwa
darasa la
kwanza, bado idadi ya watoto katika elimu ya mfumo huu usio
rasmi (MEMKWA) ni
kubwa ikilinganishwa na msisitizo wa Serikali wa kuifanya Elimu
ya Msingi kuwa bure
nay a lazima.
Amezitaja changamoto zinazoikabili Programu ya MEMKWA kuwa ni
pamoja na walimu
kukosa umahiri wa kufundisha stadi za KKK, kukosekana kwa mtaala
na miongozo ya
kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu, kutokuwepo kwa
takwimu sahihi za watoto
walio nje ya mfumo rasmi, kuchelewa kwa malipo ya honoraria kwa
walimu wa
MEMKWA, na kukosa umahiri wa upimaji na tathmini ya maendeleo ya
kitaaluma kwa
wananfunzi wa MEMKWA.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu
(ADEM), Dk.
Syston Masanja amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
iliwakabidhi Taasisi
yao (ADEM) kuratibu kazi ya mafunzo ya Wawezeshaji wa
Wawezeshaji kuhusu
uimarishaji wa Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa
Walimu wa
wanaofundisha madarasa ya MEMKWA Tanzania Bara na kwamba ‘Global
Partnership
for Education chini ya Programu ya LANES ndiyo imefadhili
uendeshaji wa mafunzo.
Aidha, amesema anatarajia mafunzo hayo yatafanyika kwa vitendo
zaidi na mbinu
mbalimbali ili kuwafanya wanafunzi watakaofundishwa kuweza
kufurahia masomo hapo baadae.
“lazima twende zaidi kwa practicals (vitendo), kwa sasa kuna
njia nyingi, teknolojia
nyingi ili anayesoma afurahie somo , tunataka mkalete matokeo
kule” amesisitiza Dk.
Masanja
Kwa upande wake , Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu (Elimu ya
Watu
Wazima) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Odilia Mushi amesema jumla ya wawezeshaji 80 watapatiwa
mafunzo ambao watakwenda kuwapatia mafunzo walimu wapatao 1594
katika vituo
vitatu vya Chuo cha Ualimu Morogoro, Chuo cha Ualimu
Tukuyu(Mbeya) na Chuo cha
Ualimu Butimba (Mwanza) lakini pia Maafisa Elimu Mikoa (Elimu ya
Watu Wazima na
Elimu Nje ya Mfumo RAsmi) watahusishwa ili kupata uelewa kuhusu
mwongozo
ulioboreshwa na kufanya ufuatiliaji.
Aidha, Mushi amesema, Nia ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kama
Serikali inataka
wanafunzi wanaochukuliwa kwa mfumo wa MEMKWA wasiwepo ifikapo
mwaka 2020
na hivyo wabakie wale tu watakao kuwa ndani ya Mfumo Rasmi wa
Elimu.
Mafunzo hayo ya walimu wa MEMKWA baada mafunzo ya siku mbili ya
wawezeshaji
yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 26 Machi, 2017 hadi 14 Aprili,
2018 ambapo mada
kadhaa zitatolewa ikiwa ni pamoja na Usimamizi na Uendeshaji wa
Elimu nje ya Mfumo Rasmi, Utekelezaji wa Mtaala ya Elimu ya Msingi kwa watoto
walio nje ya Mfumo Rasmi kwa darasa la kwanza na la pili, Maandalizi ya
Ufundishaji na Ufundishaji Kiduchu kwa darasa la kwanza na la pili, Utekelezaji
wa Mtaala ya Elimu ya Msingi kwa watoto walio nje ya Mfumo Rasmi kwa darasa la
tatu na la nne na pia Ufuatiliaji na Tathmini ya Maendeleo ya Elimu nje ya
Mfumo Rasmi.
0 comments:
Post a Comment