Na Mwandishi Wetu, Busega-Simiyu
Mkuu wa wilaya ya Busega Mkoai Simiyu Mhe. Tano S. Mwera ametumia siku ya Wanawake Duniani kuwaelimisha wanawake juu ya haki zao mbali mbali zikiwemo za mirathi, umiliki wa ardhi, pamoja na mgawanyo wa mali, pindi panapotokea wanandoa wameachana.
Mkuu huyo amesema ukatili ya kijinsia haukubaliki na adhabu kali itatolewa kwa watu watakaobainika kuwafanyia wanawake vitendo vya kikatili.
Aidha, Amewahimiza wanawake kutoa taarifa katika dawati la jinsia pindi wanapofanyiwa vitendo vya kikatili.
Vile vile mkuu wa wilaya hiyo ametumia siku hiyo ya wanawake kuzindua kampeni ya mimba za utotoni ambapo kwa sasa limekuwa janga la kitaifa.
Kampeni hiyo inakwenda kwa kauli mbiu ya " Msichana Paza Sauti" Sitaki Kuwa Mama Katika Umri Mdogo..Najitambua: Elimu ndio mpango mzima".
Kampeni hii itakuwa na waratibu kutoka kila shule za msingi na sekondari na kutoka katika makundi mbali mbali ya jamii, ambapo lengo lake ni kuwapa sehemu wasichana na jamii kwa ujumla kutoa taarifa mbali mbali za mienendo isioyofaa katika jamii ambayo inapelekea wasichana kupoteza haki yao ya msingi ya kupata elimu, ili yashughulikiwe mapema kabla ya matatizo ya ujauzito kutokea.
Pia mkuu huyo wa wilaya ya Busega Mhe Tano Mwera alisema kuwa atakayebainika kumpa mimba mwanafunzi atawekwa kizuizini kwa kifungo cha miaka 30 jela.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment