Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar,Mihayu Juma Nunga wakati akifungua Mkutano Mkuu wa baraza la Kwanza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani jana.Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Chalangwa Selemani Makwiro na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao.Picha Zote na Elisa Shunda
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kwanza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar,Mihayu Juma Nunga (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kwanza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani wakipiga kura kuwachagua wajumbe watatu wa kamati ya utekelezaji wa Mkoa huo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhani Kapeto (katikati) akishirikiana na wajumbe walioomba nafasi kuhesabu kura zao baada ya kupiga kura.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Pwani kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhani Kapeto,Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar,Mihayu Juma Nunga,Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Chalangwa Selemani Makwiro,Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Method Mselewa
NA ELISA SHUNDA,KIBAHA
VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani wahusiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusambaza habari za kusemea mambo yanayofanywa na chama hicho kwa ngazi zote zinazoratibiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar,Mihayu Juma Nunga wakati akifungua baraza la kwanza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani jana ambapo amewausia vijana hao kutumia mitandao ya kijamii katika kukisemea chama hicho pamoja na kuwasihi wadumishe upendo na kuhakikisha wanaondoa na kuvunja makundi yaliyokuwa yameundwa wakati wa kipindi cha uchaguzi ili kukijenga chama hicho.
“Kwa sasa teknolojia imekuwa kubwa sana kiasi kwamba watu mashuhuri,taasisi za serikali na binafsi zinatumia mitandao ya kijamii kusambaza kazi zinazofanywa na taasisi zao hivyo ni jukumu lenu nyinyi vijana wa uvccm wa mkoa wa Pwani mkishirikiana na Mwenyekiti wenu kuhakikisha CCM katika mkoa huu inafanya vizuri nyinyi ndo wenye jukumu la kuvuta na kushawishi vijana wenzenu na watu wengine kujiunga na chama hiki lakini pia nawahusia vijana wenzangu huu ni wakati muafaka wa kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa chaguzi mbalimbali za vijana katika chama zilizofanyika kuanzia ngazi ya Mtaa,Kata,Wilaya,Mkoa hadi Taifa” Alisema Nunga.
Aidha Naibu Waziri Nunga amewaambia vijana hao wajipange kukisaidia Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi ujao wa mwakani wa serikali za mitaa ambao ndio dira nzuri ya maandalizi ya ushindi wa kishindo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 utakaojumuisha kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge na urais.
Akizungumza katika mkutano wa baraza hilo la kwanza la Uvccm kwa Mkoa wa Pwani,Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa huo,Chalangwa Selemani Makwiro,amewashukuru wajumbe wa jumuiya hiyo ya vijana ndani ya chama kwa mkoa huo kwa imani yao kwake kwa kumpigia kura za ndiyo zilizomuwezesha akashinda nafasi hiyo ni jukumu lake sasa kuhakikisha jumuiya hiyo ya vijana inaimarisha chama kwa kuingiza wanachama wapya pamoja na kuweka mipango mikakati ili ifikapo mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa mkoa wa pwani CCM wapate ushindi wa kishindo.
“Nawashukuru vijana wenzangu wapiga kura halali wa Umoja wa Vijana CCM wa Mkoa wa Pwani kwa kunipigia kura za kutosha zilizoniwesha kupata nafasi hii ya uenyekiti wa vijana kwa Mkoa huu hivyo mimi nikishirikiana na viongozi wenzangu wa ngazi ya mkoa kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa ujao wa mwaka 2019 chama chetu kinashinda ushindi wa asilimia mia ikiwemo kurudisha na mitaa tuliyopoteza” Alisema Makwiro.
Pia Mwenyekiti Makwiro ametumia mkutano huo wa baraza kuu la kwanza la vijana wa mkoa huo kuwaomba wajumbe wa mkutano huo ambao ni wenyeviti wa uvccm wilaya,makatibu na wahamasishaji kupeleka ujumbe kwa vijana wote wanachama waliopo kwenye jumuiya hiyo kuwa uchaguzi umekwisha ni muda mzuri wa kuondoa tofauti zenu kama zipo pamoja na kuvunja makundi wafanye kazi kwa ushirikiano ili wafikie kwenye malengo waliyojiwekea umoja ni nguvu utengano ni dhaifu.
Naye mmoja kati ya wajumbe wa mkutano huo ambaye ni Mwenyekiti Wa Uvccm Wilaya ya Kibiti amesema kuwa mkutano umefanyika salama lakini pia amefarijika kuona sura mpya ya uongozi katika mkoa wa pwani anaamini viongozi waliochaguliwa wapo tayari kukitumikia chama hicho katika nafasi walizoomba ili kuhakikisha wanatatua kero za vijana na kuisimamia ilani ya chama cha mapinduzi amemhakikishia mwenyekiti wao kwenda kutekeleza yale yote aliyoyaagiza.
Pia Makatibu wa Umoja wa Vijana wa Wilaya ya Kibaha Mjini,Amina Makona na Simba M.Simba wa Rufiji wamemshukuru mwenyekiti wao wa mkoa kwa kuwaletea mhadhiri kutoka Chuo cha Diplomasia cha Kurasini ambaye katika mkutano huo alipata muda wa kutoa elimu juu ya uongozi kwa wajumbe wote waliohudhuria mkutano huo na kumuahidi kwenda kufanya kazi kwa vitendo.
0 comments:
Post a Comment