Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi
Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa
Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma leo
Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula akieleza na kufafanua masuala ya Lishe,
Uwajibikaji katika kazi na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala kwamba kila mmoja ana
jukumu la msingi katika kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma bora
kwa Watanzania, kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala
wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa
ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara
mjini Dodoma leo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi Viongozi wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Rais
TAMISEMI, pia baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi
Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa
Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara (waliosimama).
Pichani Baadhi ya Washiriki wa
kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa
Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya
kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara na Wakurugenzi wa Wizara ya Utumishi na Utawala
Bora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI
kinachofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 27 hadi 28 Februari, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe (kulia) akisikiliza jambo toka kwa Naibu Katibu Mkuu
OR TAMISEMI (ELIMU), Tixon Nzunda wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha
Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa,
Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania
Bara mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, amewataka Maofisa Elimu
nchini kote kuwa wabunifu kwa kuwapa motisha walimu katika maeneo yao ili
wafanye kazi kwa weledi.
Jafo aliyasema hayo alipokua
akifungua kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala
wasaidizi wa Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa
Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara.
Alisema kila Afisa Elimu aoneshe
uthubutu na ajipime utendaji kazi wake hali wakiangalia changamoto katika
maeneo yao na kutoa taarifa mapema ili ziweze kutatuliwa.
Alisema kwa mfano mkoa wa Dodoma
bado una shida ya elimu kwani bado haufanyi vizuri, hivyo Maafisa Elimu
wachunguze na kujua tatizo ni nini.
Aidha, alisema Maafisa Elimu
wafanye utafiti kubaini changamoto na kutafutia majibu na Ofisi yake ipo tayari
kushirikiaana nao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaofanya
vibaya katika sekta hiyo nuhimu.
“Tamisemi ipo tayari kuwasaidi,
ila hatutavumilia kama mtafanya vibaya, jukumu lenu kubwa ni kufuata miongozo
na kutoa taarifa kwa Viongozi kwani bila kufanya hivyo mtaleta mikanganyiko
katika jamii,”alisema
Pia Mhe. Jafo, aliongelea suala la
michezo kuwa serikali imeamua kuimarisha michezo katika ngazi zote, kwani
michezo na elimu vinaenda sambamba. Watoto wasioshiriki michezo mienendo yao
inakua ipo chini hivyo amewaagiza ushiriki wa michezo mashuleni.
Amewaagiza maafisa elimu
wasichague wanafunzi ambao sio wawakilishi sahihi wafuate utaratibu wa kuchagua
wachezaji kutoka shule zote.
Aliwaagiza Maafisa Elimu wajenge
utaratibu wa kujenga uzalendo kwa wanafunzi, wasisitize kuimba nyimbo za
kitaifa ili kujenga uzalendo katika nchini.
Katika hatua nyingine, Jafo
amewataka Maafisa Elimu kusimamia suala la mazingira mashuleni ili kuunga mkono
Kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais ya upandaji miti na kusaidia suala zima la
kutunza mazingira.
Amewaasa Washiriki hao kubadili
Sekta ya Elimu kwa kuboresha ufaulu hadi kufikia asilimia 80 kama sehemu ya
majukumu yao.
Naye, Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mussa Iyombe aliwataka maofisa hao kuanzia ngazi ya
kata hadi mikoa kuacha kuwatesa walimu kwa kuwa wanasababisha wajazane kwenye wizara hiyo kuonana
na viongozi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro
aliwasisitiza Maafisa Elimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi
wa Umma pamoja na maadili ya taaaluma zao kwani kumekua na malalamiko mengi juu
ya ukandamizwaji wa waalimu nchini.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu, amesema kuwabaadhi ya
Maafisa Elimu wanashirikiana na baadhi ya walimu kuhujumu vifaa vya maabara
mashuleni na kuvipeleka kwenye mashule yao binafsi na kwamba waache tabia hiyo
kwani Serikali haitowavumilia.
Dkt. Semakafu amesema Maafisa
Elimu waache uonezi kwa walimu pindi wanapotaka kujiendeleza kielimu kwa
kuwanyima fursa hiyo kwa kuwasimamishia mishahara yao bila sababu za msingi.
Awali kabla ya ufunguzi wa kikao
kazi hicho, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula
alielezea na kufafanua namna ya kuboresha masuala ya Lishe katika Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa, Uwajibikaji katika kazi kwa washiriki na
Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala (CCM) kwamba kila mmoja ana jukumu la
msingi kwa mujibu wa Ilani hiyo, katika kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma
bora kwa Watanzania na hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kufanya kazi kwa weledi,
ubunifu na uadilifu kwa maendeleo ya Watanzania.
0 comments:
Post a Comment