Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo
akizungumza na wananchi wa Makurunge katika kata ya Kiluvya wilaya ya Kisarawe.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo
akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Kiluvya B.
Wanafunzi wa Shule ya msingi Mlonganzila wakimpokea
kwa shangwe Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),
Selemani Jafo.
Wananchi wa Kiluvya B wakiwa katika mkutano walipotembelewa na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo.
...............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amewaagiza wataalam wa maji wilayani Kisarawe
kumsimamia mkandarasi wa mradi wa maji wa Kiluvya- Makurunge kukamilisha mradi
huo kwa kuondoa dosari ndogo ndogo zilizopo ili wananchi waweze kupata maji ya
uhakika.
Jafo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kuongea na
wananchi na ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Katika ziara yake, Jafo amefanikiwa kutembelea maeneo ya
Makurunge, Kiluvya na Mloganzila ambapo amekagua miradi ya elimu, afya na maji.
Akiwa katika mradi huo wa maji, Waziri Jafo amesema pamoja na Mradi
huo kukamilika lakini kuna dosari ndogondogo ambazo zinapaswa kushughulikiwa
ili maji yaweze kupatikana muda wote kwa wananchi.
Aidha Jafo amewaagiza wataalam kutembelea maeneo yao ya kazi ili
kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza hususan huduma za vyoo, maji, na
uchakavu wa miundombinu.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amechangia mifumo ya saruji 450
kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Kiluvya A na kuanza ujenzi
wa sekondari ya Mloganzila.
Aidha ameelekeza upelekwaji wa fedha za ujenzi wa vyumba viwili
vya madarasa katika shule ya msingi Mloganzila ambapo ujenzi huo
unatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment