METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, February 21, 2018

HATUHITAJI UJANJA UJANJA KWENYE BIASHARA YA MADINI

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati wa kikao na watendaji wa sekta ya madini sambamba na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Chunya akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Leo Februari 21 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Rehema Madusa akitoa taarifa ya sekta ya madini kwa Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko alipozuru Wilayani humo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Leo Februari 21 Februari 2018
Watendaji wa sekta ya madini sambamba na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa kikao cha pamoja katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Leo 21 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Mbeya

Serikali imesema kuwa zama za kufanya kazi kwa ujanja ujanja zimepitwa na wakati na hazina nafasi katika sekta ya Madini na nchi kwa ujumla kupitia uthubutu mahiri uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kurejesha weledi na heshima ya utendaji kwa watumishi wa umma, binafsi na wananchi kwa ujumla wake.

Amebainisha hayo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 21 Februari wakati wa kikao na watendaji wa sekta ya madini sambamba na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya akiwa ziarani Wilayani humo.

Alisema kuwa kama bado kuna wawekezaji, wachimbaji na wafanyabiashara wa madini wanafikiria kufanya kazi kwa mazoea na kufifihisha juhudi za serikali ya awamu ya tano wanapaswa kujitafakari upya kwani hakuna nafasi ya kufanya hivyo na endapo watatumia mbinu ovu katika utendaji wao serikali itawachukulia hatua za kisheria kwani wanarudisha nyuna muktadha wa Tanzania ya uchumi wa kati.

"Kwa muda mrefu zimefanyika biashara nyingi kwa watu wachache wasiokuwa waaminifu za ujanja ujanja zimetuumiza sana kama nchi, sasa basi" Alisema Naibu Waziri 

Alisema kuwa miongoni kwa majukumu muhimu na msimamo wa Wizara ya Madini ni kuhakikisha kuwa inawanufaisha watanzania wote sio Madini kuchimbwa Chunya lakini manufaa yake yaonekane nchi zingine duniani kabla ya ndani ya nchi.

Mhe Biteko alisema kuwa Julai Mwaka 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipeleka muswada bungeni wa marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo ni zao la Sera ya Madini ya mwaka 2009, Sera iliyokuwa na maelekezo ya ufungamanishaji wa Madini wa uchumi wa nchi.

Alisema kuwa Sera hiyo ilifungua fursa kubwa kwa wawekezaji ambapo baadaye Wizara imejiridhisha kuwa ilipelekea kuwanufaisha zaidi wawekezaji kuliko wananchi wanaoishi pembezoni mwa migodi na Taifa kwa ujumla wake.

Hivyo sheria ya madini ya mwaka 2017 ililenga hasa kuufanya uchumi wa sekta ya madini kuwanufaisha watanzania wenyewe hivyo mkazo mkubwa ni wawekezaji na wachimbaji wa madini yote kuongeza thamani ya Madini hayo hapa hapa nchini kwani kupeleka madini ghafi nje ya nchi ni sehemubya kupunguza ajira kwa wananchi.

Aidha, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Rehema Madusa kutokana na ufuatiliaji na usimamizi madhubuti wa sekta ya madini jambo ambalo alisema kuwa lina akisi ufanisi wa utendaji na dhamira ya kuwanufaisha wananchi anaowaongoza.

Sambamba na hayo pia alikitaka chama cha watafutaji na wachimbaji wa madini Mkoa wa Mbeya (MBEREMA) kutambua kuwa serikali imewapa kipaombele kikubwa ili kuongeza weledi na ufanisi wa mafanikio kwa wananchi wenyewe sio wageni.

MWISHO.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com