Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani
Jafo akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa duka maalum la dawa Kisarawe.
Mganga Mkuu wa
wilaya ya Kisarawe akitoa maelezo kuhusu uanzishaji wa duka la dawa wilayani
humo.
Stoo kubwa ya duka
la dawa Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amezitaka Halmashauri kuanzisha maduka ya
dawa katika wilaya zao ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa dawa kwenye
maeneo hayo.
Waziri Jafo ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua duka la
dawa la kisasa lililofunguliwa katika Hospitali ya wilaya ya Kisarawe ambapo
duka linatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali ya wilaya,
vituo vya afya, na zahanati wilayani Kisarawe.
Akifungua duka hilo, Jafo amesema endapo dawa zitakosekana
katika duka la hospitali au katika vituo vingine vya kutolea huduma ya afya
wilayani basi watanunua dawa katika duka hilo.
Aidha amezitaka Halmashauri zingine kuiga mfano wa Halmashauri
za Kisarawe, Muheza, Jiji la Tanga na zingine ambazo tayari zimejipanga vyema
kuwahudumia vyema wananchi wao katika suala la Afya.
Waziri Jafo ameipongeza Bohari ya Dawa(MSD) kwa msaada mkubwa
wanaoutoa katika kufanikisha uanzishaji wa maduka hayo ya dawa.
Duka hilo limeanzishwa kwa gharama ya sh. milioni 89 ambapo kiasi
cha Sh.Milioni 10 alizitoa Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe na Sh.Milioni
79 zilitolewa na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe.
0 comments:
Post a Comment