Naibu
Waziri Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa nyanya katika
Kijiji cha Ugwachanya mapema leo
Naibu
Waziri Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akishangiliwa na wakina Mama Wakulima wa nyanya
katika Kijiji cha Ugwachanya mapema leo
Naibu Waziri wa Kilimo
Dkt. Mary Mwanjelwa amepiga marufuku madadali wanaojihusisha na biashara ya
mazao ya kilimo kuwanyonya Wakulima kote nchini na kusisitiza kuwa Serikali
haitakaa iwavumilie kwani kuwanyonya Wakulima ni kosa kama yalivyo makosa mengine.
Dkt. Mwanjelwa
ameyasema hayo mapema leo katika mkutano na Wakulima wa zao la nyanya wa Kijiji
cha Ugwachanya Kata ya Mseke na Tarafa ya Mlolo mara baada ya kupokea risala ya
Wakulima wa nyanya ambao wamemweleza kutoridhishwa na mwenendo wa Kampuni ya
Darsh ambayo imekuwa ikinunua nyanya za Wakulima hao kwa shilingi 150 kwa
kilomoja.
Naibu Waziri huyo
amesema malipo ya shilingi 150 kwa kilo moja ya nyanya yapo chini sana na
kuuagiza Uongozi wa Kampuni ya Darsh kurekebisha kasoro hiyo.
Naibu Waziri huyo
hakusita kuwaeleza wazi wazi namna ambayo Serikali inavyokerwa na vilio vya Wakulima
kuhusu bei za mazao kuwa chini huku kukiwa na juhudi za makusudi za kuwalalia
Wakulima kwa visingizio mbalimbali.
“Nataka kila Mkulima
afahamu kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe
Magufuli lengo lake ni kumuinua Mkulima na kama kuna aina ya unyonyaji wa aina
hii ya kuwalalia Wakulima, haitasita kumchukulia hatua.
Kampuni ya Darsh
ilihamasisha Wakulima wa Kijiji cha Ugwachanya kulima nyanya kwa wingi katika
msimu wa kilimo ya 2016/2017 ambapo katika Kata ya Mseke Jumla ya ekari 185
zililimwa na hali hiyo ilichangia uzalishaji mkubwa na kinyume cha matarajio ya
Wakulima Kampuni hiyo haikununua nyanya sawasawa na mkataba wa awali.
0 comments:
Post a Comment