METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 2, 2018

DC HOMERA ALIFUNGA DARASA LILOANZISHWA KINYEMELA WILAYANI TUNDURU

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama wilayani Tunduru amelifunga darasa lililoanzishwa kinyemela katika kijiji cha  Chinunje kata ya Mbesa Tarafa ya Nalasi.

DC Homera alifikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa ya kwamba wananchi wamelianzisha darasa hilo lenye wanafunzi wa awali 60 na darasa la kwanza wanafunzi 185 na kuwa na jumla ya wanafunzi 245 wote wamewekwa Chumba kimoja ambacho ni kidogo na chumba hicho ni ofisi ya Chama cha mapinduzi CCM.

Wananchi hao waliamua kufanya maamuzi hayo baada ya kutaka ianzishwe shule kwenye kijiji chao na hawakutaka kutumia shule ya kijiji jirani ambayo watoto wote kuanzia darasa la pili mpaka la Saba wanasoma mpaka sasa bali darasa la kwanza wamekataa kuwapeleka katika shule mama ya chikomo na umbali wake ni mita 300 kutoka kijiji cha chinunje kwenda kijiji cha Chikomo.

Aidha, wananchi hao walidai kwamba wanaitaka shule yao kuliko kwenda kijiji jirani na hata hivyo wananchi hao wamekwisha jenga madarasa mawili kwa nguvu zao na wanataka shule yao iweze kufunguliwa kuanzia mwaka huu 2018.

Mhe Homera akiwa ameambatana na Bi Halima Nyenje Mzibiti ubora Elimu wilaya na ndg Idrisa ambaye ndiye afisa elimu alisema "Nataka wanafunzi wote waende shule mama ya chikomo ambayo ni mita 300  kutoka hapa na asiyepeleka mtoto wake shule atachukuliwa hatua stahiki"

Pia Mhe Homera alitangaza rasmi kulifunga darasa hilo huku akisema kuwa serikali itatoa jumla ya Tsh 15,000,000 na Mbunge atachangia Tsh. 5,000,000 na Bati 100  kwaajili ya kuongeza idadi ya madarasa ili kuiongezea sifa Chinunje kwa majengo waliyo jenga ili waweze kuisajili shule baada ya kukizi vigezo.

Hata hivyo wanafunzia hao kwa sasa wamerudi shule ya msingi Chikomo na wanaendelea na masomo pia na wananchi wameahidi kujitolea kikamilifu ili waweze kukamilisha ujenzi wa Shule hiyo.
MWISHO


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com