METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, February 22, 2018

CCM KIBAHA MJINI YAWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA NA UADILIFU

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini,Maulid Bundala (katikati) akizungumza na wanachama wa chama hicho wa Kata ya Visiga Mtaa wa Zegeleni wakati alipowatembelea leo. Kushoto kwake ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo,Afidu Luambano,Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi wa Kibaha Mjini,Edwin Shunda na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Visiga,Rashid Kibiriti. Picha zote na Elisa Shunda
NA ELISA SHUNDA, KIBAHA
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini,Maulid Bundala amewaasa viongozi wa serikali za mitaa wanaotokana na CCM kuwa waadilifu katika majukumu yao ya kazi wanayofanya ya kuwatumikia wananchi wa mitaa waliyochaguliwa.
Bundala aliyasema hayo leo katika ziara ya uimarishaji wa chama hicho alipotembelea Kata ya Visiga Mtaa wa Zegeleni ambapo aliwaambia wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kila kiongozi aliyepo madarakani jina lake litarudi katika mchanganuo wa kupigiwa kura kulingana na mchanganuo wa utendaji wake wa kazi kwa wananchi wake hana lawama za uuzaji wa mashamba wala uonevu kwa wananchi wake anaowaongoza.
“Kiongozi ni lazima uwe muadilifu wa utendaji kazi zako siyo kiongozi unalalamikiwa na wananchi wako wanakutuhumu unauza mashamba,kiongozi unalalamikiwa unakunywa pombe kupita kiasi unapaswa ukishakuwa kiongozi baadhi ya mambo uachane nayo kulinda heshima ya nafasi uliyonayo kwa jamii unayoiongoza viongozi ni lazima tuwe shirikishi pia tuwe mfano wa kuondoa makundi katika chama chetu ili tusonge mbele” Alisema Bundala.
Aidha Mwenyekiti Bundala amewakumbusha wanachama hao pamoja na viongozi wao kujenga mshikamano na upendo ndani ya chama hicho ambapo ndiyo nguzo kubwa ya kuwavusha katika chaguzi zijazo za uchaguzi wa serikali za mitaa hatimaye udiwani,ubunge na urais ili tushinde kwa kishindo na tuhakikishe hatupotezi mitaa,kata na jimbo kwa ujumla hivyo basi uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani ndo msingi na dira kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Hata hivyo Bundala amewashukuru wanachama wa Wilaya ya Kibaha mjini kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wao kwa awamu nyingine ya miaka mitano na amewaahidi kuwapitisha salama katika chaguzi zijazo pamoja na uimarishaji wa chama hicho kwa kuwaambia yupo katika ziara ya kata 14 za wilaya hiyo ambapo katika kata nne alizokwisha tembelea amepokea wanachama wanaotoka vyama vya upinzani takribani 50.
“Nawashukuru wanachama wa chama change kwa kunichagua tena nishike nafasi hii ya uenyekiti wa CCM Wilaya nipo katika ziara ya kutembelea kata 14 za wilaya yetu katika kata nne nilizotembelea nimepokea wanachama kutoka upinzani takribani 50 ambao wameludi CCM kutokana na utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli hivyo niwaombe viongozi wenzangu tujitoe kushirikiana na wananchi katika shughuli za kujitolea kwa mfano ujenzi wa madarasa,zahanati,barabara na kadhalika ili kuisaidia serikali katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi” Alisema Bundala.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com