Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wananchi wa Buguruni kuhusu wilaya hiyo ilivyojipanga kutekeleza maagizo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Buguruni Mnyamani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Buguruni Mnyamani.
Mafundi wakiendelea na ukarabati.
Wananchi wa Buguruni Mnyamani na Vingunguti wameanza kupata amani baada ya serikali kuanza kushughulikia barabara yao ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu kutokana na ubovu na uwepo wa madimbwi makubwa hivyo kusababisha kero kubwa ya usafiri.
Kutokana na kero hiyo,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo wiki mbili zilizopita aliamua kutembelea eneo hilo na kutoa maagizo kwamba manispaa ya Ilala, TARURA, pamoja na Dawasco kukaa pamoja na kufanya maamuzi ya haraka ili mabomba ya maji yanayo pasuka na kumwaga maji barabarani kurekebishwa haraka.
Pia aliagiza TARURA na manispaa ya Ilala kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami haraka iwezekanavyo.
Baada ya wiki mbili kupita, Waziri jafo leo ameamua kutembelea tena ili kuona utekelezaji wa maagizo yake.
Katika ziara yake, Jafo amekuta eneo lote Dawasco wamesharekebisha mabomba yao huku likiwa limebaki eneo dogo na madimbwi yaliyokuwepo awali yametoweka.
Kadhalika, Manispaa ya Ilala na TARURA kwenye mchakato wa mwishoni wa kumpata mkandarasi atakayejenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Katika ziara hiyo, wananchi wa eneo la Mnyamani ameonyesha furaha yao kwa serikali kwani kilio chao cha muda mrefu kimepata majibu ya uhakika.
0 comments:
Post a Comment