Wanafunzi wa shule ya sekondari Mibnaki wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Baadhi
ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakiwa pamoja na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea shuleni hapo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
na walimu wa Shule ya sekondari Pugu alipotembelea kukagua maendeleo ya
ukarabati wa miundombinu shuleni hapo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
na viongozi wa wilaya ya Kisarawe wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala
wa Majengo nchini(TBA) wanaofanya ukarabati wa sekondari ya Minaki.
Miundombinu ya shule ya sekondari Minaki ikiendelea
kujengwa.
Wanafunzi wa sekondari ya Minaki na Pugu wameahidi kufanya vizuri
katika mitihani yao ya kidato cha sita mwaka huu kutokana na kusomea kwenye
mazingira rafiki.
Kauli hiyo wameitoa kwa nyakati tofauti leo walipotembelewa na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akikagua maendeleo ya
ukarabati wa shule hizo.
Katika Shule ya sekondari Pugu imefanyiwa ukarabati mkubwa
katika vyumba vya madarasa, mabweni, vyoo, jengo la utawala, maabara, pamoja na
mifumo ya maji na umeme.
Aidha kwa upande wa shule ya sekondari Minaki ukarabati wake kama
ilivyo kwa shule ya Pugu na wanatarajiwa kukamilisha kabla ya mwezi Mei 2018.
Kutokana na ukarabati, Wanafunzi wa shule hizo wamemuahidi
Waziri Jafo kwamba serikali itarajie matokeo mazuri katika shule zao.
Zoezi la kuboresha shule kongwe hapa nchini limepokelewa vyema na
jamii, wanafunzi pamoja na walimu kwa kuwa lina manufaa mapana kwa maslahi ya
elimu ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment