Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
wananchi wakishiriki upandaji miti Kongwa.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi wakifurahi katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akiwa ameshika miche kwa ajili ya kupanda.
Miti inayopandwa katika wilaya ya Kongwa
........................................................................................
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde
leo amezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha
Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya KIJANISHA
DODOMA iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha
wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya
kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa.
Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya
Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali
za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mhe.
Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama
watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA
DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote
watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu.
0 comments:
Post a Comment