METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 15, 2017

UKARABATI WA SHULE KONGWE WAWAKUNA WANAFUNZI






Zoezi la ukarabati wa shule kongwe 89 hapa nchini limeonyesha kupandisha hamasa ya wanafunzi kimasomo kutokana na kubadilika kwa mazingira ya kujifunzia kuwa bora zaidi ikilinganisha hali ya awali kabla ya ukarabati huo ulipokuwa haujaanza.

Hali hiyo imebainika wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea shule ya wavulana Bwiru pamoja na shule ya Ngaza zilizopo mkoani mwanza. 

Katika ziara hiyo ,Jafo amepata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa Ngaza ambao walimhakikishia Waziri Jafo kwamba watafanya vizuri zaidi katika mitihani yao kwani kwasasa wamepata amani kubwa na hamasa tele.

Ukarabati wa shule hizo  umehusisha ukarabati wa madarasa, mabweni, vyoo, bwalo za chakula, maktaba, maabara, pamoja na mifumo ya maji na umeme.

Katika hatua nyingine,Waziri Jafo  amepongeza jiji la Mwanza kwa kuanza ujenzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya wodi ya wanaume katika hospitali ya wilaya ya Ngamagana.
Ujenzi wa jengo hilo umeanza kwa kutumia mapato ya ndani ya jiji hilo na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai 2018.

Jengo hilo linajengwa na mkandarasi Mzinga Company ambapo mpaka sasa ujenzi huo unaenda vizuri.

Katika mradi huo, Jafo amezitaka Halmashauri zingine kuiga mfano huo ili kupunguza changamoto za miundombinu katika hospitali za wilaya.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com