METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 12, 2017

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA VIWANDA AFANYA ZIARA KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

DSC_0319

Naibu waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Atembelea maonesho ya pili ya Viwanda vya Tanzania na kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwanda vya Tanzania.
Pia mhe waziri amehudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa Viwanda vya nchini ulikojadili changamoto mbalimbali za uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na kuwahakikishia wawekezaji wote wakubwa na wadogo kushirikiana na serikali katika kusema wapi wanakwamishwa ili juhudi za haraka zifanyike pale mwekezaji anapopata tatizo.
Mhe. Naibu Waziri amesema serikali inatambua umuhimu wao katika nchi hii na kuwaomba kufanya kazi kwa bidii na tija pia kulipa kodi ili kusaidia haraka maendeleo ya nchi.
Aidha Mhe. Waziri amezungumza na Waandishi wa habari na kueleza jinsi alivyojionea maonesho haya ambayo yamekuwa mfano kwa nchi yetu kwa kuwaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji wote.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com