METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, December 23, 2017

MWIGULU AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO LONGIDO

Comrade Dr.Mwigulu Nchemba amezindua kampeni za Chama cha mapinduzi katika uchaguzi mdogo  jimbo la Longido unaotarajiwa kufanyika january 13 2018.

Comrade Nchemba  amewataka wananchi wa jimbo la Longido  kumchagua mgombea wa CCM Dr Steven Kiruswa awe mbunge wao kutekelza ilani ya chama mapinduzi kwa kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.

Comred Mwigulu amesema wapinzani wameogopa kuwa  wataachwa mbali katika baada ya kupima uitikio wa wananchi ambao wanakubali kazi za Rais Dr John Maguful na serikali ya chama cha mapinduzi ambayo inatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na wananchi wanaona.

Comrade Dr Mwigulu  amewahakikishia wananchi wajitokeze siku ya kupiga kura kwani usalama ni wa uhakika wakati wa kupiga kura.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com