Naibu Waziri Wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Ghala la
Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe
wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017. Picha Zote Na
Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe
wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la
Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe
wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la
Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe
wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Na Mathias Canal, Njombe
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu
juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji
kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.
Mradi huo utahusisha ujenzi Wa Vihenge vya kisasa, Maghala ya
kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo baada ya mradi huo kukamilika wakala
utakuwa umeongeza uwezo Wa kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya
Tani 250,000 ambapo Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.
Mradi huo unataraji kutekelezwa na kampuni mbili za kandarasi
kutoka serikali ya Poland (Feerum na Unia Arab) kwa usimamizi Wa Wakala Wa
Majengo Tanzania (TBA) ambapo unataraji kugharimu zaidi ya Bilioni 150 za
Kitanzania.
Tayari maandalizi ya awali yameshakamilika ikiwemo Utiwaji saini
mikataba, Uchunguzi Wa udongo, Tathmini ya athari ya Mazingira, Pamoja na
kutembelea eneo la mpango kazi.
Akizungumza wakati akikagua Ghala la Kuhifadhia mahindi Kanda ya
Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
alisema kuwa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umefanya kazi kubwa
ya ubunifu na kujiongeza kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima katika Kanda zote
saba ikiwemo ya Makambako-Njombe, Kipawa-Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga,
Arusha, Songea na Sumbawanga.
Alisema kuwa pamoja na Kanda ya Makambako kupangiwa kununua
jumla ya Tani 6500 katika msimu Wa mwaka 2017/2018 ambapo baada ya lengo
kukamilika ziliongezwa fedha za ununuzi hivyo kununua jumla ya Tani 8,961.530
Akisoma taarifa ya Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba alisema kuwa Kanda ya
Makambako ni miongoni kwa Kanda itakayoongezewa uwezo Wa kuhifadhi ambapo
tayari kuna kiwanja chenye ukubwa Wa Hekari 2,9965 kilichopo Makambako na Mbozi
chenye ukubwa Wa Hekari 53.691.
Alisema Wakala umefanikiwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni
pamoja na kununua baadhi ya Mazao ya Chakula cha ziada kutoka kwa wakulima,
Kutoa Chakula cha ziada kwa waathirika, Kutekeleza mkakati Wa kukuza uchumi na
kupunguza umasikini (MKUKUTA) kwa kutoa bei nzuri kwa wakulima wanaouza Mazao
yao kwa NFRA sambamba na utekelezaji Wa malengo ya milenia 2025.
Katika ziara hiyo ya kikazi ya Siku Moja katika Mji Wa Makambako
Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Kilimo pia amekutana na kufanya kikao cha kazi
na wafanyakazi Wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya chakula Kanda ya Makambako
ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kufanya kazi kwa Nidhamu, Weledi,
Kujituma, Uvumilivu, Bidii na mshikamano.
Wakati huo huo amefanya mazungumzo na wakulima kutoka Kanda ya
Makambako ambapo wakulima hao wamesifu Juhudi za serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwa kuwajali ikiwa ni pamoja na kupunguza Tozo na Ushuru.
Wakulima hao kwa nyakati tofauti wameupongeza Uongozi Wa Wakala
Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Makambako kwa kuwashirikisha na
kuwajali wakulima katika kila hatua ya ununuzi Wa mazao.
Utekelezaji wa Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi mazao kwa Vihenge vya kisasa, Maghala na ukarabati wa ofisi utaanza Disemba 8, 2017.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment