METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 22, 2017

JAFO AKERWA NA UCHAFU SOKO LA MABIBO




WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na uchafu uliokithiri katika soko la Mabibo lililopo wilayani Ubungo jijini  Dar as salaam. 

Soko hilo maarufu kwa jina la Mabibo-mahakama ya ndizi limetapakaa maji machafu na madibwi yanayotoa harufu mbaya.   

Jafo amesema uchafu huo ni hatari sana kwa afya ya wananchi kwani wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu.

Kutokana na hali hiyo, Jafo ameielekeza manispaa ya ubungo kufanya marekebisho ya haraka ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi na kusambaza kokoto sokoni hapo pamoja na kuweka mfereji wa kupitishia maji.

Pia Jafo amewataka watendaji wa soko hilo kusimamia mapato ipasavyo kutokana na ukusanyaji mapato kuwa hauridhishi.

Amesema  wastani wa sh.milioni 90 kwa mwezi zinakusanywa ikilinganishwa na biashara kubwa ya ndizi na viazi inayofanywa sokoni hapo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com