METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 23, 2017

VIKUNDI 40 VYA WAJASIRIAMALI VIJANA NA WANAWAKE HALMASHAURI YA CHALINZE WILAYANI BAGAMOYO VYAPATIWA SHILINGI MILIONI 120

1
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na vikundi mbali mbali vya wajasiriamali  havipo pichani  kutoka halmashauri ya Chalinze katika halfa fupi ya  makabidhiano ya hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120 ambayo itaweza kuwasaidia katika kufanya biashara zao.
2
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu akizungumza jambo na vikundi vya wajasiriamali ambao walifika katika sherehe hiyo ya makabidhiano ambayo ilifanyika katika viwanja vya sokoni Lugoba
3
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga kulia akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120  mmoja wa wanakikundi wajasiriamali katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya soko la Lugoba
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
……………..
NA VICTOR MASANGU, LUGOBA BAGAMOYO

KATIKA  kukabiliana na wimbi la umasikini na  ukosefu wa ajira kwa  vijana pamoja na wanawake hatimaye  halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani  imeamua kuvipatia  mikopo wa kiasi cha shilingi milioni 120 Vikundi 40 vya wajasiriamali  kutoka kata 15 kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika halfa ya makabidhiano  ya hundi kwa ajili ya fedha hizo iliyofanyika katika kata ya Lugoba  Mkuu wa  Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufui  ni kuhakikisha inawawezesha kiuchumi wananchi wake pamoja na kuwapatia mikopo ya fedha  kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

Aidha Mwanga aliwaagiza watendaji na viongozi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu vikundi vyote ambavyo vimeshakopeshwa kufanya ukaguzi wa kina  kujua fedha amabzo zimetolewa zinatumika katika matumizi sahihi kwani amebaini kuna baadhi yao wanakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa  hivyo kurudisha nyuma kasi ya  maendeleo.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Mohamed Sume  akisoma taarifa yake  amebainisha kuwa fedha hizo zote zimetokana na makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani  kwa lengo la kuweza kuviwezesha vikundi hivyo ikiwa ni kutekeleza Agizo la  ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kutenga asilimia kumi kwa ajili ya kuwawezesha vijana pamoja na wanawake.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu amesema kuwa fedha ambazo zimetolewa katika vikundi  vya wajasiriamali hao ni katika kota ya kwanza  ambapo pia wametenga  milioni 300 kwa lengo la kuweza kuvipatia vikundi vingine ili kuweza kuongeza pato la Taifa kupitia biashara wanazozifanya.

Alisema kwamba mipango ya halmashauri hiyo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 vikundi vyote vya ujasiriamali vinawezeshwa kwa kupatiwa mikopo ya kufanyia biashara zao mbali mbali sambamba na kuwapatiua wataalamu ambao watakuwa wakiwafundisha namna na kuweza kujifunza masuala mbali mbali yanayohusina na namna na kuweza kutafuta masoko katika bidhaa wanazozizalisha.

Baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na fedha hizo akiwemo Zawadi Rashid pamoja na Mwajuma Shaban  walieleza malengo na matarajio yao  ni kuhakikisha wanakuza mitaji yao kwa kuendeleza biashara  walizonazo, ikiwemo ufugaji, kilimo, ufyatuaji wa matofali pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo ili kuweza kujikwamua kimaisha na kukuza uchumi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com