Na Mwandishi Wetu, Simiyu
Jana Novemba 28, 2017 Umoja wa Wanawake Wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoani Simiyu umefanya uchaguzi maalumu Wa Jumuiya hiyo katika nafasi mbalimbali za ngazi ya Mkoa na Taifa.
Mkutano huo maalumu Wa UWT umechagua viongozi watakaohudumu katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017-2020 kwa mujibu Wa katiba ya CCM.
Uchaguzi huo umesimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega , Mhe Tano Mwera, Katibu wa Ccm wilaya ya Meatu ndugu, Charles Mazuri kwa niaba ya Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu ndugu, Donard M. Etamya.
Katika uchaguzi huo Bi Mariamu Manyangu aliibuka mshindi kwa kupata kura 234 hivyo kuwa Mwenyekiti wa Umoja Wa Wanawake Wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) huku Bi Tinna Chenge akichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza kuu la UWT taifa baada ya kupata kura 294.
Wajumbe wa baraza La UWT Mkoa kutoka Wilaya ya Meatu walichaguliwa Bi Agnes Marwa kwa kura 330 na Bi Salina Omary kwa kura 316 ambapo Wajumbe wa baraza UWT Mkoa waliochaguliwa kutoka wilaya ya Bariadi ni Thereza Mponya kwa kura 222, na Winfrida Masanja kwa kura 178.
Baraza LA UWT Mkoa kutoka Itilima walichaguliwa Bi Paulina Dotto kwa kura 306 na Lucia Say kwa kura 233 ilihali kwa upande wa Baraza la UWT Mkoa kutoka wilaya ya Maswa walichaguliwa Bi Joyce Mashauri Ndaki kwa kura 268 na Bi Fatuma Masele kwa kura 261.
Baraza LA UWT Kutoka wilaya ya Busega katika Mkoa walichaguliwa Bi Zainabu Karama aliyepata kura 172 na Janeth Vian kwa kura 145. Na Mjumbe Mkutano mkuu Mkoa alichaguliwa Bi Esther Manyama kwa kura 152.
Mjumbe Mkutano mkuu UWT kwenda Mkutano mkuu wazazi alichaguliwa Bi Amina Hasani kwa kura 129 huku Mjumbe wa UWT kwenda Mkutano mkuu wa Vijana(UVCCM) Mkoa alichaguliwa Bi Thekla Stephano kwa kura 134.
Mwisho wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Busega aliwashukuru wajumbe wote kwa kufanya uchaguzi kwa hali ya usalama na amani na kuwapongeza wote waliochaguliwa na kuwataka kutokuwa mizigo bali wale wafanye kazi kwa bidii chini ya kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu na CCM Mpya Tanzania Mpya.
Mhe Kiswaga pia aliwapongeza waliochaguliwa na kuwatakia majukumu mema katika ustawi na uimarishaji Wa Chama na Jumuiya zake katika usimamizi Wa ilani ya Uchaguzi ili kumsaidia kutekeleza majukumu ya kikazi Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Mhe Kiswaga aliwasihi viongozi waliochaguliwa kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Mkoa sambamba na ngazi zingine ngazi ya Taifa kuvunja makundi yote yaliyokuwepo kabla ya uchaguzi.
Mwenyekiti Mstafu Bi Averina Kyakwambala aliwashukuru wajumbe wote kwa kufanya nae kazi kwa ushirikiano katika kipindi chake chote wakati akiiongoza Jumuiya hiyo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment