METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 25, 2017

SHAKA ANENA MAZITO UFUNGAJI WA KAMPENI KATA YA NANGWA

#"Miaka 25 ya uwepo  wa vyama vingi vya upizani CCM haikuyumba wala kutetereka, upizani ulianza kwa udhaifu na utamaliza ukiwa dhaifu kwa kuwa hawana mipango wala mikakati ya kuvijenga vyama vyao na kuwa taasisi kamili za kisiasa kama kilivyo Chama Cha Mapinduzi " Shaka  

#"Vyama bora vya siasa ni lazima viwe na katiba, miuundo bora ya uongozi na sera zinazojali maslahi ya umma na kutetea wananchi wanyonge na masikini kama kinavyofanya chama cha Mapinduzi kilichotokana na  vyama vya vya  TANU na  ASP" Shaka 

#"Mhe  Magufuli,  mhe  Samia,  mhe majaliwa, mama Nagu  wote waliandaliwa na kupikwa na CCM na leo  ni viongozi wanalitumikiaTaifa  na Portajia ameandaliwa na amewiva na sasa yuko tayari kuwatumia wana  Nangwa  mpeni kura kesho" Shaka.

#"Nawapongeza vijana wenzangu  kwa kukataa kunasa katika mtego siasa za ghiliba na hadaa za vyama vya upizani ambavyo vilikusudia kuwapotosha vijana kuwapumbaza kifkra na kujaribu kuwaondolea uaminifu utii na uzalendo wa kulitumikia taifa lao" Shaka

#"Nazungumza na watanzania kupitia wananchi wa Nangwa  nikiwaeleza  kwamba upizani hauwezi kusimama na kukubalika mbele ya watanzania kwa kuwa vyama hivyo vimeundwa na  viongozi waliofukuzwa CCM  aidha kwa usaliti, ukuwadi wa kisiasa au kushiriki kwao katika vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma." Shaka

#"Aina ya viongozi kama hawa wakubaliki katika mbele ya watanzania vipi wataungwa mkono na kuwaamini kuwapa kura " Shaka

#"Chama hiki CCM  ndicho chama  kilichowakomboa watanzania na sehemu kubwa katika bara la Afrika, chama hiki ndicho alichotoka Baba  wa  Taifa  Mwalimu  Julius  Kambarage Nyerere ndicho alichotoka Rais wa  kwanza  wa  Zanzibar  na mpigania uhuru wa  Afrika hayati   Mzee Abeid  Amani  Karume" Shaka

#"Ndicho chama  alichotoka  Mzee Rashid  Kawawa Simba wa  vita, Mzee  Thabit  Kombo, Mzee Msekwa, hayati Aboud Jumbe  Mwinyi  na viongozi wengine  waadilifu, waaminifu, na wazalendo halisi ambao hawana tuhuma za unyonyaji, dhulma ama kushiriki ufisadi" Shaka

#"Wananchi na wakaazi wa  kata  ya  Nangwa kesho mkimchagua  Portajia kuwa diwani wenu mtakuwa hamjapoteza lolote bali mtakuwa mumeendelea kuwaenzi na kuwaheshimu wapigania uhuru wa Taifa  letu " Shaka 

#"Kwa bahati mbaya hata viongozi wa upizani  walioshiriki kuviunda vyama hivyo wamekata  tamaa wamevipuuza  na wengine wameamua kufanya maamuzi sahihi kurudi CCM"    Shaka 

#" Rais Magufuli alitembea nchi nzima kunadi ilani  ya uchaguzi ambayo sasa tunaitekeleza kwa mafanikio makubwa kwa Jimbo la Hanang anasaidiwa na Mama Merry Nangu  mpeni na Portajia waungane watatu kuleta maendeleo endelevu  kiuchumi na kijamii  Nangwa na  Hanang  kwa ujumla" Shaka

#"Sifa kubwa ya  CCM ni kuandaa  viongozi wazuri mama Portajia ana uwezo mkubwa katika kutenda mpeni aje ashirikiane na Mbunge kutatua kero ya maji , Barabara na kukamilisha shule mlizojenga kwa nguvu zenu" Shaka

#"Bahati mbaya kwa miaka 7 mumeteseka na upizani   mkombozi wenu ni Portajia wa CCM  mchagueni kesho, achaneni na hao matapeli wenzi wa asilimia 5 za vijana na wakinamama ameiba hata calvat zilizotolewa kwa ujenzi wa Barabara na kuenda kuuza" Shaka

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com