Nzega Mjini, Tabora.
Hivi Karibuni nikiwa kwenye ziara jimboni kwangu nilipata heshima ya kutembelewa na Waziri wa Maji *Mheshimiwa Mhandisi Kamwele*. Kwa pamoja tulipata wasaa tukaaa pamoja na timu ya wataalamu wa wizara kujadili utekelezaji wa Mradi wa maji ya Ziwa Victoria unaoendelea kwa sasa; ambapo kwa kina tuliweza kujadili mapungufu yaliyojitokeza na mahitaji halisi.
Nitumie Fursa hii kuishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dk. John Pombe Magufuli* kutokana na namna ambavyo amekua mstari wa mbele kushirikiana nasi kutatua kero kubwa ya maji katika Jimbo la Nzega Mjini.
Aidha, Katika majadiliano yetu nilimueleza Mheshimiwa Waziri mapungufu makubwa ya maji kwenye maeneo ambayo Mradi hautafika na kipekee napenda kuishukuru kwa dhati Serikali kwani tulifikia Muafaka kutatua changamoto hiyo kwa kuanza Utekelezaji wa Mradi mkubwa wenye thamani ya pesa za kitanzania Bilioni Moja (Tzs 1,000,000,00) unaohusisha upanuzi wa miundombinu ya maji kwa maeneo ambayo hayatafikiwa na Hatua ya Kwanza Maji ya ziwa victoria.
Pamoja na hilo Tutachimba Visima virefu 13 vya kutumia Teknolojia ya nishati ya Jua (Solar energy).
Visima hivi vitahudumia maeneo ambayo Mradi wa maji ya ziwa Victoria hautafika kama ifuatavyo;
(a) Kijiji cha Nhobola - visima 2
(b) Kijiji cha Igilali - Visima 3
(c) Kijiji cha Iyuki - Visima 2
(d) Kijiji cha Kitengwe - Visima 2
(e) Kijiji cha Idudumo - Visima 2
(f) Kijiji cha Mwanzoli - Visima 2
Kwa muda mrefu Maji yamekua ni changamoto kubwa sana katika Jimbo la Nzega Mjini na Nzega kwa ujumla lakini hatua hii ni muhimu na tayari tenda ya visima 13 imeishatangazwa.
Narejea kumshukuru waziri kwa kupita katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini; na pia namshukuru kwa jitihada zake binafsi alizoonyesha kukutana na Wataalamu wa Maji wa halmashauri ya mji wa Nzega.
Nimuhakikishie waziri na serikali kuwa mradi huu tutausimamia kikamilifu kwa ajili ya mafanikio na matokeo yaliyokusudiwa na kuwa mfano wa miradi mingine mingi ya Maji nchini.
Imetolewa na;
*Mhe. Hussein M. Bashe (Mb)*
*Nzega Mjini*
0 comments:
Post a Comment