Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza jana Jijini
Dar es Salaam na Wakuu wa Taasisi za Serikali kuhusu Kampeni ya
Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za
Serikali Bw. Geofrey Mwambe kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
(aliyesimama )akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na
Wakuu hao kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa
mwezi ujao Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiwaonyesha Wakuu wa
Taasisi za Serikali Jarida la Nchi Yetu linaloelezea mafanikio ya miaka
miwili ya Serikali ya awamu ya Tano lililondaliwa na Idara yake kwa
kushirikiana na Taasisi hizo jana Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.
Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa
na Michezo imeandaa Kampeni ya “Uzalendo na Utaifa” inayotarajiwa
kuzinduliwa Disemba nane mwaka huu Mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lengo ikiwa ni
kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto
zilizojitokeza na zitakazojitokeza katika Taifa letu.
Akizungumza na Wakuu wa Taasisi
za Serikali jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Kampeni hiyo
inadhamiria kuwakumbusha watanzania Utamaduni wetu na Uzalendo
uliokuepo miongoni mwa Watanzania ambao ulileta heshima kubwa ndani na
nje ya nchi.
“Kampeni hii ina lengo la
kurudisha Uzalendo tuliokuwa nao Watanzania katika kuheshimu mali za
Umma, kuogopa rushwa,ubaguzi wa kidini,kikabila,kiitikadi na kikanda
ambavyo vilianza kupotea,lakini Serikali ya awamu ya Tano imeanza
kurudisha hivyo sisi kama watanzania tunapaswa kuunga mkono jitihada
hizi”Alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha Dkt. Mwakyembe ameeleza
kuwa Kampeni hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya ikiwemo kurejesha na
kuimarisha moyo wa Uzalendo na Utaifa kwa Watanzania hususan vijana na
watoto umuhimu wa kuipenda na kuithamini nchi yao pamoja na kuimarisha
umoja upendo na mshikamano wa kitaifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Wakuu wa Taasisi za Serikali kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Bw. Geofrey Mwambe amesema Taasisi za Serikali zinaunga mkono Kampeni
hiyo kwani itasaidia watanzania wengi kuelewa historia na Utamaduni ya
nchi yao na kuitilia maanani popote watakapokuwa.
Kampeni hiyo yenye kauli mbiu
“Nchi Yangu Kwanza” itakuwa ni endelevu na inatarajiwa kufanyika kila
mwezi Oktoba kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba
wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
0 comments:
Post a Comment