METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 25, 2017

HABARI PICHA MHE NEEMA MGAYA KAKITOA MISAADA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Josephat Kandege (Kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA wakati wa hafla ya kuhitimisha mpango wake wa kugawa vyerehani 370 kwa akinamama, vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari 105 za Mkoa huo iliyofanyika Wilayani Ludewa.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Kulia) akifurahi jambo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Josephat Kandege mara baada ya kuwakabidhi vyerehani baadhi ya wanawake wa Wilaya ya Ludewa ikiwa ni vyerehani 370 alivyogawa kwa akinamama wa Mkoa huo.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Kulia) akimwelekeza jambo Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Ludewa Thomas Kiowi namna ya kuwatafutia masoko akinamama waliokabidhiwa vyerehani kupitia mpango wake wa kugawa vyerehani 370 kwa akinamama, vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari 105 za Mkoa huo.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Kulia) akimkabidhi Kepteni wa timu ya wanawake ya Mapinduzi Quuen ambao ni washindi wa michuano ya Soka za wanawake mkoani humo jozi ya jezi tukio ambalo limeendana na ugawaji wa vyerehani kwa wanawake wa wilaya ya Ludewa  ikiwa ni mpango wake wa kugawa vyerehani 370 kwa akinamama na vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari 105 za Mkoa huo.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Kulia) akimkabidhi Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ludewa MATERNUS NDUMBARO baadhi ya vitabu vya ziada ambavyo ametoa na kufanya idadi ya Shule zote za Sekondari za umma na mbili za kidini ambazo zimepatiwa vitabu hivyo katika Wilaya za Wanging’ombe, Makete, Njombe na Ludewa mkoani Njombe kufikia 105. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Josephat Kandege na Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com