MANUFAA
ya uchumi unaokua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati wa viwanda
hayataonekana kama taifa litakuwa na changamoto katika utengenezaji wa
miji yake na hivyo kuvuna tija ya miji iliyopangwa vyema.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya
Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy wakati akifungua mkutano wa
wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania
(Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF).
Mkutano
huo ulikuwa na lengo la kuangalia mada tatu zilizokubaliwa kufanywa
kama sehemu ya kutengeneza mwongozo wa namna ya kuendesha mpango huo ili
kuisaidia serikali katika kutengeneza miji salama na yenye tija.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa wanazuoni walio
katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania)
unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Mada
hizo tatu ni pamoja na kuangalia miundombinu ya miji na huduma za
kifedha katika utengenezaji wa miji, mahusiano ya serikali kuu na ya
mitaa ; na mada ya tatu ni namna ya kupata taarifa sahihi ili kuimarisha
uwekezaji.
Kessy
alisema wakati serikali inatekeleza malengo ya mpango wa pili wa
maendeleo wa miaka mitano (FYDP) ll , wenye lengo la kuweka mazingira
sawa kwa uchumi wa viwanda na maendeleo, mpango huo wa ESRF umekuja muda
muafaka kwani utasaidia kutafuta na kutoa majawabu halisi na sahihi.
Kaimu
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka
Paul Kessy akifungua mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira
za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi
ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema
kwamba kama nchi itataka kuwa na maendeleo yenye kujali binadamu ni
vyema kuwa na maamuzi ya miongo yenye kuakisi uhalisia na mahali pekee
kwa sasa kupata huo uhalisia ni wa kutumia mpango huo wa ESRF ambapo
wanazuoni watakutana kujadili uhalisia wa mambo na kutoa mapendekezo ya
kukabili changamoto.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida alisema mkutano huo ambao ni
wa kwanza tangu alipoamua kuwa na Tanzania Urbanisation Laboratory,
Agosti mwaka huu umelenga kusaidia kutengeneza njia ya kusaidia
utengenezaji wa miji salama yenye tija nchini.
Alisema
kwa kuwa mwenyekiti wa mpango huo ni Tume ya Mipango wao wakiratibu tu,
ni dhahiri mawazo na mapendekezo yatakayokuwa yanatolewa kulingaana na
utafiti yatasaidia sana kuwa na miji salama.
Pichani
juu na chini ni Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika
iliyopo Afrika Kusini, akitoa mada ya utangulizi wakati wa mkutano wa
wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania
(Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Mtafiti
kutoka ESRF, Jires Tunguhole (kulia) akiwasilisha mada kuhusu kuwelewa
upangaji wa miji na namna fedha zinavyopatikana wakati mkutano wa
wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania
(Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dr. Wilfred Lameck, akiwasilisha mada Utafiti
kuhusu mahusiano ya serikali kuu na serikali za mitaa Tanzania wakati
wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa
Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Dr.
Nathalie Jean-Baptiste kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu
katika Chuo Kikuu cha Ardhi, akiwasilisha mada kuhusu maisha ya kila
siku ya watanzania katika miji wakati wa wa mkutano wa wanazuoni walio
katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania)
unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.Pichani
juu na chini ni washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa wanazuoni
walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab
Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Kaimu
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka
Paul Kessy akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika
Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania)
unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida.Mtafiti
Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akifafanua jambo wakati wa
mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa
Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Dr
Kate Owens kutoka World Resources Institute ya Marekani akitoa neno
wakati wa kufunga mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za
Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Pichani
juu na chini ni washiriki wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango
wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na
taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (kushoto) akibadilishana mawazo na Bw. Anton Cartwright (katikati)
kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini pamoja Dr. Kate
Owens kutoka World Resources Institute wakati wa mkutano wa wanazuoni
walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab
Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.Picha
ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa
Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na
taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment