Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imetoa orodha ya awamu
ya tatu ya wanafunzi 7,901 wa mwaka wa kwanza watakaopata mikopo.Taarifa
iliyowekwa kwenye tovuti ya bodi na kuthibitishwa na Meneja Mawasiliano
wa HELSB, Omega Ngole imesema hadi sasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza
waliopata mikopo ni 29,578. Bodi ilisema jumla ya wanafunzi 30,000
watapata mikopo hiyo.Katika awamu ya kwanza wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipata mikopo na awamu ya pili wanafunzi 11,481 walipata.Ngole
akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Novemba 5,2017 amesema orodha ya
wanafunzi waliopata mikopo inapatikana www.heslb.go.tz.Amesema bado bodi inaendelea kuchambua majina ya wanafunzi wengine walioomba na taarifa zitatolewa baadaye.
Malunde
0 comments:
Post a Comment