METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, October 24, 2017

TAMASHA LA MPIRA WA KIKAPU KWA VIJANA MWANZA LAFANA

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameshiriki kama mgeni rasmi katika Tamasha la mpira wa kikapu kwa vijana jijini Mwanza lililofanyika katika uwanja wa mpira wa kikapu Kiloleli likihusisha vijana wenye umri wa miaka 14-16  kwa ushirikiano wa Taasisi inayojishughulisha na Michezo ya PSD na Chama cha mpira wa kikapu mkoani Mwanza MRBA

Akizungumza katika viwanja hivyo Mhe Dkt Angeline Mabula amewaasa vijana hao kutumia michezo mbali na kuimarisha afya zao kiwe chanzo cha kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao
‘.. Michezo sasa si sehemu ya kujenga afya tu bali iwe chachu ya kuwainua kiuchumi  katika kuongeza kipato chenu ..’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewahakikishia vijana hao kuendelea kuwaunga mkono katika kuboresha Michezo na kuifanya kuwa ajira ikiwa ni muendelezo wa mpango mkakati wa kupambana na changamoto ya ajira sambamba na harakati za kuinua Michezo ndani ya Jimbo lake la Ilemela

Mbali na hayo Mhe Dkt Angeline Mabula amekabidhi mipira 10 kwa Timu shiriki za mchezo huo na Jezi kwa Makocha wa Timu hizo

Kwa upande wake Afisa Elimu na Michezo wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Kizito Bahati mbali na kumshukuru Mhe Dtk Angeline Mabula amemuhakikishia kuendelea kushirikiana na Ofisi yake katika kutimiza adhma ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli ya kuboresha michezo nchini sanjari na kuifanya kuwa sehemu ya kuboresha maisha ya wananchi

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
24.10.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com