Yamkini umeshawahi kusikia kwamba wanaume hukosa uaminifu kwa sababu za
kimwili zaidi wakati wanawake nao hukosa uaminifu kwasababu za kihisia.
Nikweli kuwa upo ukweli katika hilo, ingawa katika utafiti huu wanawake
mbalimbali walipoulizwa kwanini walijiingiza katika mahusiano yasiri
mbali na wapenzi wao walikuwa na sababu tele zakuelezea, wako
walioelezea kuwa walikuwa wanafurahisha hisia zao tu na wengine walikuwa
kwenye mkakati wakulipiza kisasi kwa kile walichowahi kufanyiwa na
wapenzi wao, na sababu nyingine nyingi zilielezwa.
Jaribu kusoma kwa umakini ili ufahamu nini walikisema na kilichowafanya
kujiingiza katika majaribu hayo. Ni matumaini yangu kwamba utakutana na
sababu nyingine ninazokusibu au zilizowahi kukusibu wewe, na yamkini pia
ukapata kufahamu kwanini mambo fulani yanaendela vile yalivyo.
Kukosekana kwa mvuto
Mmoja wa waliohojiwa anasema “Nilikuwa na mpenzi wangu kwa muda wamiaka
mitatu, alikuwa kijana mzuri sana na nilifurahia sana ninapokuwa naye
lakini tatizo nikwamba hakukuwa na chembe ya mvuto baina yetu. Wengi wa
marafiki zetu walikuwa wameshachumbiana na kuvishana pete lakini kila
mchumba wangu alipojaribu kuanzisha hoja ya kunivisha pete nilijitahidi
sana kubadilisha mazungumzo ili tu tusiklizungumzie hilo.
Ipo siku nilisafiri kikazi na huko nikakutana na na kijana mfanyakazi
mwenzangu ambaye taratibu nilijikuta naanza kuvutiwa nae. Kwakweli
ulikuwa wakati mzuri sana, labda kwasababu niliitarajia safari hii kwa
muda na nilikuwa sijasafiri kwa muda pia na ukizingatia nimekutana na
mtu ninaevutiwa nae basi mambo yalikuwa mazuri zaidi.
Wakati wa kurudi ulipofika nilirudi nyumbani nikatengana na mchumba
wangu na kujikuta sasa naanza mahusiano rasmi na yule kijana
niliyefanyanae kazi kule nilikoenda. Ingawa siwezi kusema najisifia kwa
nilichokifanya, lakini namshukuru Mungu kwamba mambo yaliendelea kuwa
mazuri upande wangu kwa sababu mimi na yule kijana tuliamua kuoana na
hadi sasa tunaishi kwa furaha na mapenzi mazuri”.
Kuchelewesha kitendo cha kuachana
“Kabla tu sijaenda kuachana na mwanaume aliyekuwa mpenzi wangu,
niligundua kuwa alikuwa na hali mbaya sana kihisia, hakuwa tayari kabisa
kusikia kwamba tunaachana nahii ikanifanya kukosa ujasiri wa kumtamkia
kuwa tuachane. Kwahiyo nikasubiri kama mwezi mmoja hivi ili haliyake
irudi kuwa njema ndiyo nimwambie.
Mara tu haliyake ilipokuwa sawa na wakati na mimi nimeshaanza kupata
ujasiri wa kumwambia mara akafukuzwa kazi, nikajihisi tena nimerudi
katika hatua ya kwanza. Wakati huo sasa tayari nilishakutana na kijana
ambaye nilishatamani sana kuanza naye mahusiano, na kwa kushindwa
kujizuia na kwahali niliyokuwa napitia kimahusiano nikajikuta
nimemruhusu awe mpenzi wangu, pasipo hata kumhusisha mpenzi wangu wa
awali kuwa sasa nipo katika mahusiano mengine.
Nahisi nilijipamoyo kwamba siwezi kumwambia sasahivi wakati hali yake
yakihisia haikuwa nzuri”. (Binti aliyehojiwa hapa alikuwa na miaka 30,
wakati yule wa kwanza alikuwa na miaka 33)
Madhara ya kuwa mbali na mpenzi wako
“Mimi na mchumba wangu tuliamua kuendelea na mapenzi yetu tukiwa
mbalimbali mara tu nilipopata nafasi ya kwenda chuo kikuu mbali na
nyumbani. Miezi michache ya kwanza haikuwa na shida, kila kitu kilikuwa
sawa na tuliwasiliana bila shida.
Lakini kila muda ulipokuwa ukienda nikajikuta naanza kuvutiwa na kuwa
karibu na kaka mmoja aliyekuwa mwanafunzi mwenzangu na mara kwa mara
nilikutana naye maabara za sayansi. Baada ya masomo kumalizika nilirudi
nyumbani na nilimkuta mchumba wangu akinisubiri kwa hamu sana. Kwakweli
kukaanae kipindi hiki haikuwa rahisi kabisa ingawa sikuweza kuachana nae
wakati huu sababu bado nilivutiwa nae.
Ziko nyakati hapa katikati nilimtembelea yule mwanafunzi mwenzangu
niliyevutiwa nae tukiwa chuoni na nikagundua kuwa kilichokuwa baina ya
mimi na yeye kilikuwa ni hisia zaidi nasio penzi haswa, ingawa
tulishajikuta tukiingia katika penzi, nahisi hii yote ilisababishwa tu
na upweke na kuwa mbali na mwenzangu, basi nikaamua kuacha kabisa
kuwasiliana na yule mwanafunzi mwenzangu na kuweka mawazo yangu yote kwa
mpenzi wangu kwasababu nilijua kuwa yeye ndio alikuwa wangu wa maisha,
nasikitika kwamba sikuwahi kumwambia kilichoendelea wakati nikiwa
chuoni, ingawa maranyingine najihisi kushtakiwa moyoni. Maranyingine
najipa moyo kwamba ule ulikuwa utoto na ujinga tu. Sasa mimi nayeye
tunaendelea vema na ni miaka mine sasa tangu nimemaliza chuo kikuu”.
Kuepukana na kuwa mpweke
Binti huyu mwenye miaka 28 anasema “Nilianza tu kuhusiana kimapenzi na
kijana niliye naye sasahivi mara baada ya kuachwa na mpenzi niliyekuwa
naye kwa miaka miwili.
Kwakweli ilikuwa ngumu sana kwangu na huyu mpenzi wa sasa kweli
aliniokoa katika maumivu hayo, baada ya mimi nayeye kuwa katika
mahusiano kwa miezi mitano hivi, mpenzi wangu wa kwanza akarudi na
kuomba nimruhusu na kumpa nafasi tena na kuahidi kuwa hayatotokea tena.
Ukweli ni kwamba bado nilihisi kumkosa sana moyoni mwangu, kwahiyo
tukaanza kuonana mara kwa mara ingawa sio kwamba nilikuwa nimeachana na
huyu niliyekuwa naye sasa.
Najihisi nilikuwa nimemuweka huyu kijana wa sasa karibu ili
kujihakikishia usalama zaidi maana sikuwa nikijiamini sana kuwa na yule
wa awali, nilihofia kama ataniacha tena angalau ninamtu pembeni yuko
tayari kwa ajili yangu, ingawa sio kwamba nilimpenda kiukweli kama
mpenzi wangu wa mwanzoni.
Kwa bahati mbaya mimi na mpenzi wangu wa awali hatukuweza kuendelea vema
hata baada ya kumpa nafasi ya pili aliyoiomba, mbaya zaidi nikwamba
mpenzi wangu wa sasa alipogundua kuwa nilikuwa ninaonana mara kwa mara
na yule wa kwanza na yeye akasema hatoweza kuendelea na mimi. Kweli
nilijifunza somo hapa kuhusu kuhusiana na wanaume wawili wakati mmoja,
na pia kujifanya najaribu kulea nakubembeleza penzi lililokwisha kufa”.
Kutafuta pumziko baada ya mahusiano mabaya
“Nilipokuwa binti mdogo (sasa hivi nina 30) nilikuwa katika mahusiano na
kijana mmoja ambaye kwakweli alikuwa akinipinga katika kila
ninachokifanya, alinikejeli sana kuhusu maumbile yangu na uzito wangu,
mara aseme mimi mjinga, mara sijui kitu, mara mi mshamba na mambo
mengine mengi mabaya.
Pamoja na mabaya yote haya bado niliamua kuwa naye tu ingawa marafiki
zangu wote na wazazi na ndugu zangu walimchukia. Siku moja nikiwa kwenye
sherehe nikakutana na kijana mmoja na gafla tulijikuta tumezama kwenye
maongezi ya mapenzi na hisia zetu kuvaana. Yani huyu alikuwa ni tofauti
kabisa na mpenzi wangu, wametofautiana kilakitu kuanzia maneno hadi
matendo, yani ni kijana mpole, mzuri wa tabia, mkarimu na ananitia moyo
badala ya kunivunja moyo.
Mara kwa mara tulikuwa wote tukifurahia siku za mwisho wa wiki,na moyoni
mwangu ikawa kama vile taa ya yule wa kwanza ndiyo imezima kabisa. Kwa
mara ya kwanza nilimbusu usiku kabla hajaondoka kurudi nyumbani kwao, na
nilipoenda kuonana na yule wa kwanza nilimwambia tuachane. Niliamua
kuendelea sasa rasmi katika mapenzi na mpenzi wangu mpya na baada ya
miaka mitatu tukaamua kuoana”.
Jitihada za kutafuta kile unachohisi kukikosa
“Mimi ni binti niliyekulia katika mikoa ya pwani kwahiyo napenda sana
kwenda fukweni kukaa, kuogelea na kupunga upepo. Kwa bahati mbaya mpenzi
wangu amekulia zaidi bara kwahiyo mambo ya fukweni kwake sio kitu
kabisa na hapendi, mara kwa mara tumekuwa na ushindani na mikwaruzano
kuhusu wapi twende tukapumzike na mara zote yeye ndio anashinda.
Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi nane, kuna wakati
nilisafiri mimi na rafikizangu na tulitumia boti kwa muda mrefu wa
safari, nahodha wa boti hii alikuwa kijana mzuri, mtanashati na
anaonekana ni mtu wa maisha ya fukweni zaidi, kweli nilivutiwa nae,
Tulipofika tuliahidiana kuonana usiku ule na tulikuwa na wakati mzuri
sana pamoja, sikuwahi kumwambia mpenzi wangu kuhusu yaliyoendelea katika
safari yangu, na wala sijihisi kushtakiwa moyoni mwangu, tena kuna
maranyingine najihisi ndani yangu kuwa kile ndicho kilikuwa chema
kumfanyia huyu mpenzi wangu kwasababu ya utukutu wake.
Bahati mbaya sana mimi na mpenzi wangu hatukuweza kuendelea sana,
tuliachana baada ya mimi kushindwana naye na niliamua kuhakikisha kwamba
kila kijana nitakayeamua kuhusiana naye basi lazima ayajue maisha ya
fukweni”.
Jitihada za kumuadabisha (kumkomesha)
“Mpenzi wangu wa mwisho alikuwa na tabia za wanawake sana kabla
hatujaamua kuanza neye mahusiano, nilidhani ningeweza kumbadilisha tabia
yake hiyo lakini nilijidanganya, mara kwa mara nilisikia tetesi kuwa
alikuwa anaonana na wasichana wengine wakati bado tuko naye katika
mahusiano, lakini kila nilipomuuliza marazote alikataa katakata.
Usiku mmoja nilipata simu kutoka kwa msichana ambaye walikuwa
wamehusiana naye kwa miezi mitatu na akaniambia kuhusu msichana mwingine
pia ambaye na yeye amegundua kuwa anamahusiano na huyu mpenzi wangu.
Nilikuwa na hasira sana usiku ule, niliamua kutoka na marafiki zangu
nikiwa nimevalia mavazi ya kumvuta kila mwanaume ambaye aliniona, na
nikaamua kuwa na muda na kijana fulani mzuri sana niliyekutana naye
katika mtoko ule.
Ndani yangu nilipata kupumua kidogo nikajihisi kuwa angalau hicho ndiyo
alichostahili mpenzi wangu huyu, nilitamani na nilifurahia kuuona uso
wake jinsi anavyokuwa wakati nikimpa taarifa ya nilichokifanya usiku ule
na ninayoyajua kuhusu yeye na wanawake zake na hatimaye nikamwambia
kila mtu achumue muda wake, na tukaachana”.
Friday, October 27, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
-
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 4, 000,000,000/= kutoka kwa Meneja Mkazi (Country Manager) wa Kampuni ya Madini ya...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea k...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment