





Meneja wa
Global Publishers, Abdallah Mrisho, jana (Jumamosi, Sept. 30,2017)
alifunga ndoa ya kifahari na Catherine Mdamu, iliyolifanya Jiji la Dar
es Salaam lisimame kwa muda, ikifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Katika
sherehe hiyo, wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na
mkurugenzi wao, Eric Shigongo, jamaa na marafiki, walijumuika kula,
kunywa mpaka kusaza na kucheza muziki mzuri, mpaka usiku sana huku
kukiwa na ‘special appearance’ ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
0 comments:
Post a Comment