METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, October 4, 2017

MKOA WA ARUSHA WAJIZATITI KUKAMILISHA ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

DSC04223
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akiwa kwenye kikao na Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kujadili kuanza kwa zoezi la Usajili Wilayani humo.
DSC04346
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Viola Lazaro Likindikoki alipokutana na watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kujadili mpango wa Usajili kwenye Halmashauri hiyo.
DSC04352
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ndugu David Mwakiposa akizungumza na Viongozi wa NIDA walipotembelea ofisi yake leo kukamilisha mpango wa Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi na wageni wanaoishi mkoani humo.
DSC04357
Kamishna Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha Bw. Ali Mohamed akisikiliza kwa makini mpango wa utekelezaji zoezi la Usajili wananchi mkoani humo wakati alipokutana na Viongozi NIDA na kukubaliana mpango wa pamoja wa utekelezaji wa zoezi hilo.
……………..
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.  Gabriel Fabian Daqarro ameuhakikishia Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) dhamira waliyonayo ya kuhakikisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea waishio mkoani humo hususani katika Wilaya ya Arusha wanasajiliwa Vitambulisho vya Taifa kwa wakati uliopangwa.

Kauli hiyo ameitoa leo alipokutana na uongozi wa Mamlaka, kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuendesha zoezi hilo ambalo litaanza rasmi katika Wilaya hiyo Ijumaa Kata za Sekei, Themi na Sombetini.

Katika awamu hii ya kwanza takribani wananchi 45,000 watasajiliwa. Ametoa wito kwa wadau wote wakiwemo viongozi wa Dini, wanasiasa na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanasaidia kuhamaisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi hili ambalo lina manufaa makubwa katika maendeleo ya Taifa. Aidha; ameonya zoezi hilo kuhusishwa na siasa.

Naye Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Viola Lazaro Likindikoki ameahidi ofisi yake kwa kuhusisha wadau muhimu kushiriki kikamilifu kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, na kwamba wakazi wa jiji  hilo wanahamasishwa kushiriki.

Viongozi wengine waliopata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na uongozi wa NIDA ni Naibu Katibu Tawala wa Mkoa huo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Arusha Bwana Ali Mohamed. Wilaya zingine za Mkoa wa Arusha tayari zimeanza zoezi la Usajili zikiwemo Monduli, Arumeru na Karatu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com