Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager
Marathon zimezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Chama Cha Riadha
Tanzania, wadhamini na waandaaji. Akizindua mbio hizo, Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na michezo Mh. Dk. Harrison Mwakyembe alisema
Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa maandalizi yake
ni mazuri na kuwataka waandaaji wa mbio nyingine kuiga mfano huu.
“Tunataka kuwaibua kina Felix Simbu wengine na hili linawezekana tu
kupitia mbio kubwa kama Kilimanjaro Marathon. Nimefahamishwa kuwa Simbu
pia alitokana na mbio hizi kwani aliwahi kushiriki kilometa 21 miaka ya
nyuma...sisi kama serikali tutafanya kila linalowezekana kuyafikia
malengo haya,” alisema.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison
Mwakyembe akitoa hotuba wakati wa uzinduzi rasmi Mbio za 16 za
Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 uliofanyika jijini Dar es
Salaam. Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alitoa rai
kwa washiriki kuhakikisha wanajiandikisha mapema li kuepuka usumbufu
dakika za mwisho na kutoa mfano wa mwaka huu ambapo namba za ushiriki
zilikwisha kutokana na watu wengi zaidi kujitokeza. “Tumeshazungumza na
waandaaji ili kuwepo na namba za kutosha mwakani,” alisema. Alisema
ujumbe mkuu wa Kilimanjaro Premium Lager kwa mbio za mwakani ni ‘Kunywa
kistaarabu usiendeshe ukiwa umekunywa’.”Najua wengi tungependa kufurahia
kili zetu baridi baada ya mashindano lakini tunywe kwa ustaarabu,”
alisema huku akiongeza kuwa zawadi kwa mshindi wa kilometa 42 ni milioni
4 kwa mwanaume na mwanamke na jumla ya zawadi ni milioni 20 kwa
washindi wote.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis akizungumza kuhusu
udhamini wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018
zitakazofanyika mwakani Machi 4 mkoani Kilimanjaro. Kushoto Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli na Kulia ni Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe. Kaimu
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini,,Henry Kinabo alisema, “Tuna
furaha kuwa sehemu ya mbio hizi kwa mara nyingine. Hizi ni mbio ambazo
zinawaleta pamoja wanariadha wakubwa na watu kutoka Nyanja mbalimbali
kusherekea michezo, kufurahi, kukuza utamaduni, utalii na pia kwa afya
bora,” alisema. Alisema Tigo, inayodhamini mbio za kilometa 21, itatoa
jumla ya Milioni 11 kama zawadi huku msindi wa kwanza wa kiume na kike
wakijinyakulia milioni 2 kila mmoja wa pili milioni 1 wakati wa tatu
watapokwa Tsh 650,00o huku Katia ya 500,000 na 100,000 zikienda kwa
washindi kuanzai wan ne hadi wa 10 pamoja za medali za ushiriki kwa kila
atakayemaliza mbio.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli (wa tatu
kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa sherehe za uzinduzi wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager
Marathon jijini Dar es Salaam. Meneja Masoko wa TBL anayesimamia
kinywaji cha Grand Malt, Warda Kimaro, alisema mbio za Kilometa 5
zinazodhaminiwa na Grand Malt zinakuwa mwaka hadi mwaka na kuwavutia
watu wengi zaidi wakiwemo watoto, vijana na watu wazima. “Tumeandaa
shughuli mbalimbali za kusisimua kwa ajili ya washiriki kwa hivyo
tujiandikishe mapema na tukumbuke kunywa Grand malt kwa kuwa ni kinywaji
chenye afya hasa kwa wanariadha,” alisema. Kilimanjaro Premium Lager
Marathon huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media na kuratibiwa
na Executive Solutions. Wadau wengine muhimu ni, Chama Cha Riadha
Tanzania, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Kilimanjaro Marathon
Club, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,vilabu vya jogging na Jeshi la
Polisi.
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo (kulia)
akizungumzia jinsi kampuni yake ilivyojipanga kutoa huduma mwakani
katika mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018
zitazofanyika mwakani machi 4 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Meneja Masoko wa TBL Group anayesimamia Grand Malt, Warda Kimaro
(kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi
wa Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe
akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za 16 za
Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitazofanyika machi 4 mjini
Moshi, mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe. na Kushoto ni Mkurugenzi wa
Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis.
Pichani juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mh. Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akizindua rasmi mbio za Kilimanjaro
Premium Lager Marathon 2018 leo Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka
kushoto ni Meneja Masoko wa TBL Group anayesimamia Grand Malt, Warda
Kimaro, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, Katibu
Mkuu wa TOC Filbert Bayi, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo, Alex
Nkenyenge, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli,
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis na Makamu wa Rais wa
Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na wadhamini wakuu TBL.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison
Mwakyembe katika picha ya pamoja na wadhamini wa meza za maji mbio za 16
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitakazofanyika machi 4
mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Wednesday, October 25, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza itakayotumika kutibu endapo ata...
-
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Rukwa (hawapo pichani) Wakuu wa taasisi mba...
-
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCI), Robert Boaz Mikomangwa amesema Jeshi la Polisi nchini Tanzania na vyombo vingi...
-
Na Dotto Mwaibale KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment