Afisa
elimu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na washiriki wa mkutano
uliowakutanisha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule binafsi (TAMONGSCO), Charles Totela Akizungumza
Miongoni mwa wamiliki wa shule binafsi pamoja na wawakilishi waliofika kwenye mkutano huo
Na Michael Utouh
AFISA
Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu ameahidi kutatua kero zote
zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsiinafsi wa mkoa huo
ikiwemo ya tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule hizo .
Pia
amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee
kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa
kuwa wana walimu wengi wa masomo hayo.
Ameyasema
hayo leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu uliowakutanisha wadau
mbalimbali na wamiliki wa shule zilizopo mkoani humo.
Amesema
wamiliki wa shule hizo pamoja na shule zao wanapaswa watambaue huduma
wanazopewa ni stahiki hivyo ni sawa wanazopatiwa shule za Serikali.
“Natamani
kuziona shule zote binafsi zikiwa zinazoongoza kutokuwa na changamaoto
zozote kwani tunatambua mchango wa uwekezaji hapa nchini,” amesema.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi
nchini (TAMONGSCO), Charles Totela ameishukuru Serikali ya mkoa huo
kwani imekuwa ikiwapa ushirikiano wa kutosha.
Mwenyekiti
huyo ameiomba Serikali ya mkoa huo kuwaundia dawati la pamoja
litakalowakutanisha viongozi wote wa shule binafsi, za serikali na
watendaji wao ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana baadhi ya
changamoto ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi.
Naye
Mkurugenzi wa Shule za Al-Muntazir, Mahmood Ladack amewashukuru
wamiliki wa shule hizo kwa kuhitisha mkuatano huo ambao anataraji
utakuwa na manufaa makubwa kwao na taasisi wanazosimamia katika
kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment