METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 13, 2017

SHAKA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA PANTALEO RUMANYIKA WILAYANI MULEBA

13/09/2017 Mkoa wa Kagera

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo jioni ameongoza mamia  ya waombolezaji, wanafamilia, ndugu, jamaa, wanachama wa CCM na wananchi mbali mbali katika mazishi ya Katibu wa UVCCM wilaya ya Hai Pantaleo P. Rumanyika aliyefariki kwa ajali Ijumaa iliyopita.

Marehemu Pantaleo P. Rumanyika amezikwa leo  kijijini  kwao Bulamula Kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera.

Viongozi wengine waliodhuria ni  Mkuu wa Wilaya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Makatibu wa CCM wilaya na mikoa na jumuiya zake kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Geita, Kagera, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba pomoja na maafisa mbali mbali wa Chama na jumuiya zake.

Marehemu Pantaleo Rumanyika amezaliwa 1972 kijijini  Bulamula Wilaya ya Kagera, ameajiri Umoja wa Vijana wa CCM mwaka 2001 amefanya kazi katika vituo mbali mbali ikiwemo Misenyi,  Biharamulo, Ngara, Dodoma vijijini, Mbongwe, Nyangwale, Bukombe, Bukoba Mjini na hadi mauti yanamfika alikuwa wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro

Marehemu ameacha Mke na watoto 3 wakike 2 , mwanaume 1 na wajukuu 3.

Bwana ametoa, bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.

Amina

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com