METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 4, 2017

SHAKA: CCM IPO SALAMA CHINI YA JPM

"Chama cha siasa ni kama mti ambalo ikiwa shina litaimarika na kuwa madhubuti bila shaka matawi ya mti huo yatastawi na kunawiri wakati wote aidha ikiwa ni nyakati za kipupwe kiangazi au masika" Shaka

"Chama Cha Mapinduzi kipo katika mikono salama ya uongozi wa Mwenyekiti CCM Dk John Magufuli na Katibu Mkuu wake Kanali Mstaafu Adulrahman Kinana chama hicho kitazidi kuimarika kuanzia ngazi ya mashina hadi Taifa na kuendelea kushinda katika chaguzi mbali mbali" Shaka

"Nina  uhakika uhai wa CCM na maendeleo yake kisiasa yameongezeka maradufu kuliko miaka ishirini iliopita hivyo hakuna chama chochote cha upizani kitakachokitikisa chama cha Mapinduzi au kukiyumbisha." Shaka

"Chama makini cha siasa kama CCM huongozwa na katiba, kanuni, miongozo na sera hivyo huwezi kuilinganisha ccm na vyama vingine ambavyo licha ya kukosa misingi imara ya demokrasia na nidhamu lakini pia havina viongozi makini" Shaka

"Waswahili wanasema siku zote ukiona matawi ya mti yamepooza ubovu upo shinani." Shaka

" CCM haitathubutu hata siku moja kuwapuuza mabalozi wa nyumba kumi, viongozi wa mashina na matawi kwani uhai wa chama  upo katika mikono kwenu na ninyi ndio chachu ya ushindi wetu na ndio maana leo tumekutana kusikiliza mipango yenu ya ushindi na tushauriane kwa pamoja" Shaka

'Rais Dk Magufuli na Mzee Kinana wamekipa heshima chama kwa kufanya kazi ya kupigwa mfano leo  CCM ni kioo cha siasa na demokrasia Afrika. Kazi yao katu haitafutika kwenye kurasa za historia ya ccm na maendeleo yake na ndio maana yapo matumaini makubwa kushinda kwa kishindo chaguzi hizi za marejeo " Shaka

"CCM inayotokana na vyama vya TANU na ASP ambavyo ndivyo vilivyoleta uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wake ndiyo waliweka misingi ya usawa, haki, kupiga vita ukabila, udini na ukanda hivyo wana ccm hawatakubali kuiacha nchi mikononi mwa wanasiasa mafisadi na wahuni." Shaka

"Wapo viongozi wa upinzani walioshindwa kufanya siasa na kuwashawishi wananchi ili wawaunge mkono badala yake sasa wameanza kuleta chokochoko ili kuhatarisha amani na utulivu uliopo."  Shaka

"Walianzisha umoja wa demokrasia (Udeta) ukafa, wakaja na Ukawa wakagawanyika, wakabuni ukuta ukavunjika, operesheni sangara wakazama nayo ziwani na sasa wameamua kubeba makapi wakidhani yatawatasaidia chaguzi hizi za marudio nadhani tutawapa funzo tosha na itakuwa ni dalili njema ya mafanikio ya CCM kuelekea 2020"  Shaka

"Uzembe wa chadema katika kukosa kwao weledi katika upimaji, upembuzi na uchambuzi wa masuala ya kisiasa hukisaidia chama cha mapinduzi kujipanga zaidi kwani kila wanapokubali kuramba matapishi yao wananchi huwashangaa." Shaka

"Chadema hutoa shutuma nyingi kuwa mwanasiasa fulani ndani ya serikali ni fisadi na mbadhirifu, ccm ikianza kumbana mwanachama huyo kupitia vyombo maalum vya kiusalama, anapokosa maelezo na kukimbia fedheha wao humdaka na kuona huo ni ushindi kwao " Shaka

"Kitendo cha chadema kukubali kukaribisha mafisadi na kuwapa uongozi wa juu huwavunjia heshima ya
kisiasa na kuonekana chama hicho kina upungufu mkubwa wa wanasiasa mahiri na wenye upeo wa mbali."  Shaka

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com