METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 7, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA KISWAHILI ZANZIBAR



Na Kudra Mawazo, Zanzibar

Makamo wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassain amesema kuwa uwepo wa kamisheni ya kiswahili hapa Zanzibar ni moja ya heshima ilopata zanzibar kwakuwa ndio kitovu cha kiswahili barani Afrika.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kiswahili la kimataifa ambalo linafanyika Zanzibar kwa siku tatu katika hotel ya Golden Tulip iliyopo malindi unguja.

Kongamano hilo limeudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka katika jumuiya ya afrika mashariki na nje ya ,jumuiya ya afrika mashariki,ambapo samia alizindua mpango mkakati wa kamisheni hiyo wa miaka mitano (2017-2022).

Samia amesema kuwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wapo tayari kutenga bajeti kwa lengo la kuendeleza kamisheni hiyo,kwakuwa umuhimuwa kamisheni hiyo ni mkubwa kwa kukuza lugha ya kiswahili katika mataifa ya afrika na duniani kote.

Alisema kuwa dira ya EAC 2050 inalenga kuongeza kasi ya utengamano wa kikanda,ambao ni umoja wa forodha,soko la pamoja,sarafu moja na ushirikiano wa kisiasa, na kuifanya kamosheni hiyo kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kukitangaza kiswahili na kutoa fursa kwa mataifa yalio nje ya kumuiya ya afrika mashariki kujifunza kiswahili na kuwa na tafsiri moja ya maneno mapya ya kiswahili.

Alisema lunga ya  kiswahili ni kiungo muhimu katika kufikia malengo hayo ambayo itasaidia kujenga utambuzi na kubaini changamoto na fursa zinazofungamana na maendeleo hayo.

Samia alisema kuwa tanzania ipo tayari kutoa walimua wa kiswahili kwa taifa la sudan ya kusini kwa lengo la kufundisha kiswahili katika nchi hiyo baada ya kutoa maombi ya kupatiwa walimu wa kswahili.

Sudani kusini ni nchi ya sita ambayo imejiunga na jumuiya ya afrika mashariki mwaka 2016,taifa hilo ni taifa ambalo kiswahili ni lunga mpya kwa wanachi wao.

Mapema kaimu mwenyekiti wa baraza la mawaziri la umoja wa afrika mashariki balozi Dk Augustine Mahiga alisema kiswahili ni miongoni mwa lunga Zinazokuwa kwa kasi duniani na kubainisha haja ya kuiendeleza ili kutimiza lengo la kuwaunganisha wananchi wa ukanda wa afrika mashariki.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com