Diwani
ya Kata ya Mabibo (aliyefungwa kitambaa machoni), akipelekwa na MC wa
shughuli hiyo, Chaku kwenda kuchagua kuponi ya ushindi.Mheshimiwa diwani akiwa kwenye rundo la kuponiMheshimiwa diwani akichanganya kuponi.
Kazi ya kuchanganya kuponi ikiendelea.Mheshimiwa diwani akiwa ameshika kuponi ya ushindi, iliyotoka Gazeti la Championi.Mheshimiwa diwani akiwa ameiinua kuponi juu.Diwani Lema akisoma jina la mshindi wa nyumba, aliyemshikia kipaza sauti ni MC Chaku.Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza kwenye droo hiyo kubwa ya Shinda Nyumba.Meneja Mrisho akipeana mikono na Diwani LemaDiwani Lema akizungumza na watu waliofika kushuhudia droo hiyo.Msomaji akichagua kuponi ya mshindi wa zawadi ya dinner set.Msomaji akichagua kuponi ya mshindi wa zawadi ya dinner set.Mhariri wa Uwazi, Elvan Stambuli (kulia) akiwa na mhariri mwenzake, Sifael Paul anayesimamia Gazeti la Ijumaa Wikienda.Abdallah
Hemed (kushoto), afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, akiandika
jambo huku akifuatilia droo hiyo, pembeni yake ni Meneja Mrisho.
Hatimaye Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba iliyokuwa ikiendeshwa kwa
zaidi ya miezi 6 na Kampuni ya Global Publishers ikiwa ni sehemu ya
kurudisha fadhila kwa wasomaji wake, imefikia mwisho ambapo mshindi
kutoka Dodoma amepatikana.
Katika droo ya fainali hiyo, ambayo imefanyika kweNye Viwanja vya Las
Vegas, Mabibo jijini Dar huku mgeni rasmi akiwa Diwani wa Kata ya
Mabibo, Kassim Lema, mshindi aliyejishindia nyumba hiyo iliyopo Bunju B,
nje kidogo ya Jiji la Dar, ni George Majaba mkazi wa Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza na Gazeti hili, mapema baada ya kumaliza shughuli ya
kumtangaza mshindi wa nyumba hiyo, Meneja Mkuu wa Global Publishers,
Abdallah Mrisho aliwashukuru wasomaji wa Magazeti ya Global kwa kuwa
waaminifu katika kipindi chote ambacho wameshiriki kimamilifu kwenye
kinyang’anyiro cha kumpata mshindi.
Mbali na mshindi huyo wa nyumba, pia kulikuwa na washindi wengine
walioibuka na zawadi za dinner set, ambao ni Kahabi Suleiman wa
Vingunguti, Dar, Melania Swai wa Mbezi, Dar na Philemon Faustine wa Dar.
0 comments:
Post a Comment