Na Tiganya Vincent-Tabora
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wote wa umma kuondoka
maofisa na kwenda vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za
wananchi ambazo yanasababisha wasiendelee.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana wakati akiongea na watumishi wa Wilaya ya Uyi mkoani Tabora.
Alisema kuwa wakisha kuwasiliza wananchi
warudi Ofisi kwa ajili ya kujipanga namna ya kutatua kero na matatizo
ya wananchi ambayo yanakwamisha juhudi zao ya kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya
Tano ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote na hivyo imetoa dhamana
kwa watumishi wa umma wafanye kazi karibuni kwa kwenda vijijini ili
kuwatumikia Watanzania wote.
Aidha alionya kuwa Serikali hii
haitawavumilia watumishi wa umma wenye tabia za urasimu katika
kuwatumikia na kutatua kero mbalimbali za watanzania.
“Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote
wa umma ambayo mwananchi anakwenda kwake kwa mara ya kwanza kueleza
shida yake kisha anamwambia mwananchi arudi kesho na anaporudi kesho ,
anambia tena arudi kesho …..mwisho mwananchi anaanza kukata tamaa ya
kusaidiwa tatizo lake” alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema kuwa mwanachi anapofika katika
Ofisi za Umma kwa ajili ya kutatuliwa tatizo lake asaidiwe haraka bila
kuzungushwa zungushwa ili aone Serikali yake ipo kwa ajili ya kumsaidia.
0 comments:
Post a Comment