Askari wa Minusma, kikosi cha Umoja wa Mataifa Mission nchini Mali, katika mji wa Timbuktu, Septemba 19, 2016.
Nchini
Mali, siku moja baada ya kifo cha askari wa Ufaransa aliyeuawa katika
mlipuko wa bomu la ardhini kaskazini mwa nchi hiyo, shambulizi jingine
jipya lililenga Jumapili hii kikosi cha Umoja wa Mataifa kiliyotumwa
nchini humo. Askari mmoja alipoteza maisha na saba kujeruhiwa, huku
watatu wakiwa ni katika hali mbaya.
Shambulizi
hili lilitokea kaskazini mwa mji wa Douentza, karibu na kijiji cha
Bambara Maoudé katikati mwa Mali. Msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa,
uliyokua ukishindikizwa na askari wa kulinda amani, ulikanyaga mabomu
mengi ya ardhini. Shambulizi hili lilifuatiwa na urushianaji risasi.
Inaarifiwa kuwa washambuliaji hao walikua wakisubiri msafara huo. Askari walijibu haraka, na kuwatimua washambuliaji hao.
Umoja wa
Mataifa ulituma helikopta zake za kivita, lakini kutokana na hali ya
iliyokua ukijiri katika eneo la shambulizi, helikopta hizi
iliwasafirisha majeruhi hadi hospitali. Kwa mujibu wa Minusma, askari wa
kikosi hiki kutoka Togo alifariki muda mfupi baada ya kuwasili kwa
askari wengine waliokuja kusaidia, askari wengine saba walijeruhiwa,
ikiwa ni pamoja na watatu ambao wako katika hali mbaya. Wote
walisafirishwa katika mji wa Timbuktu.
0 comments:
Post a Comment